Raha ya vijijini ni chakula fresh kutoka shambani. Hapo juu Ankal akiwa Kiwira akiburudika na 'mabifu', na chini  akitoka shambani  kuchuma miwa huko Tukuyu, mkoani Mbeya

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 18 mpaka sasa

  1. Ndio maana huzeeki kula starehe za kijiji huku ughaibuni tukivipata hivyo vimejaa madawa!!

    ReplyDelete
  2. Ankal,kuuvuna muwa sio kuungowa na mizizi yake. Hukatwa ili miche myengine ihuwike. Au hupendelei na wengine kuja kuupata utamuuuu.

    ReplyDelete
  3. Labda ughaibuni ya afghanistan,i live in USA and fruits r juat as natural as they could get,acheni uongo

    ReplyDelete
  4. Mbona hukuvaa kauka nikuvae yako leo?

    ReplyDelete
  5. Kijijini kungekuwa na nyumba nzuri umemme na maji, mvua ikinyesha chakula fresh kipo.

    ReplyDelete
  6. Ankal naomba kuuliza,,,, huo Mua ume ungóa au ume uchuma?

    ReplyDelete
  7. Ankali unatia hasara. Wewe umengoa kabisa. Muwa unakatwa na kuacha shina lake ili liendelee kuzaa.

    ReplyDelete
  8. Wewe mdau namba tatu huko US hakuna hivo vitu fresh unavyotutambia.

    Vimewekwa madawa vikue vizuri na vionekane ni fresh, kama una ujuzi wa kilimo utaelewa hivyo.

    ReplyDelete
  9. Huyo mdau wa tatu Ame comment ili kuonyesha na yy yupo States; But in fact chakula fresh ni moja ya vitu ambavyo wadau wa Ughaibuni tunavikosa. Nikiwemo mm mdau wa Canada.

    ReplyDelete
  10. Nukuu"Kijijini kungekuwa na nyumba nzuri umemme na maji, mvua ikinyesha chakula fresh kipo."

    Wewe kaa tu huko, watu wanajenga vijijini kwao na ni kuzuri.

    LABDA NI KUULIZE UNATOKA KIJIJI GANI? UNACHEKESHA KWELI.

    ReplyDelete
  11. Haya ndio mambo yanayotufanya tutake raia mbili ili tufaidi kotekote.....wee miaka sita sasa sijala mua...unafanya mchezo nini...

    ReplyDelete
  12. Ankal,kule uswahili wanasema "Tam ya muwa kifundo" hivi mswahili wewe umeligundua hilo . Kama bado basi ule kwanza ukesha libainishe hilo ankal.

    ReplyDelete
  13. muwa na mambo ya uraia pacha wapi na wapi? Kama una uraia wa nchi nyingine bado ni ruksa kuja bongo kutembea au hata kuishi (wapo raia kibao wa nchi nyingi wanaishi kwa vibali)sasa wewe iweje miaka sita hujatembelea bongo na unaanza kulaumu kuwa inatokana na kukosekana kwa uraia pacha???

    ReplyDelete
  14. Huu si uvunaji ni uharibifu. Muwa unakatwa siyo kung'olewa

    ReplyDelete
  15. Uncle Issa, wajuwa ,fani za Muwa ni nyingi.Jee wewe huo wakwenda kuutengeneza Juice, au wakusudia kuufanya sukari gulu au gendeli au uwaumenya tu ukesha uufyonze lakini kuwa na hadhari utam usijeukakumwaikia tu maana raha ya muwa ndio itapote.

    ReplyDelete
  16. Basi Ankal nikushangaze.Nguruwe wanapenda sana miwa.Lakini waiila huwa hawasimami,isipokuwa huila au kuifyonza utam wake wakiwa wamelala chali,ili kila tone la utam liwafike ndipo yaani lisimwaike.Amini huwalala Chali,chali hasaaaaaaa!hahahaaa.

    ReplyDelete
  17. KWA MHUSIKA,
    Kwa Kiswahili barabara, Mtu hachumi muwa...bali anatoka kuvunja muwa; kukata muwa au kuvuna muwa.

    Kazi njema.

    ReplyDelete
  18. Mjomba Michuzi,

    Afadhali yako umebakia kuwa na Utanzania wako!

    Angalia hapo ahhh mwenyewe upo kule Gairo-Morogoro Picha ya juu unakula ndizi mbivu na Picha ya chini mwenyewe na muwa wako begani upo shamba Kijijini!

    Neema ya Utanzania na maisha simple ambayo ndugu zetu wengi walisha ipoteza na sasa wanaililia wakati maji yamesha mwagika na hayazoleki!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...