Na Mwene Said wa Globu ya
Jamii, Mahakamani
Mtu mmoja raia wa Kenya Nelson Onyango (43), mkazi wa Kariakoo, jijini Dar es Salaam, amefikishwa katika Mahakamani akikabiliwa na mashitaka saba ya udanganyifu, kutumia kadi zisizosajiliwa, kuingiza nchini na kutumia mitambo ya simu bila kibali, kutoa huduma ya mawasiliano ya kimataifa bila kibali cha Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na kuisabishia serikali na mamlaka hiyo hasara ya Sh. Milioni 6.8.
Onyango alisomewa mashitaka yake leo mbele ya Hakimu Mkazi Devota Kisoka aliyepangiwa kusikiliza kesi hiyo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam.
Jamhuri imewakilishwa na Mawakili wa Serikali Mwandamizi, Tumaini Kweka, Mwanaamina Kombakono na Mwanasheria Mkuu wa TCRA, Joannes Karungura na Inspekta wa Polisi, Jackson Kinunda.
Mheshimiwa Kweka alidai shitaka la kwanza, kati ya Julai mwaka 2010 na Novemba mwaka 2013, eneo la Kariakoo wilaya ya Ilala, jijini, bila halali na kwa makusudi mshtakiwa akiwa na nia ya kukwepa malipo halali alitoa huduma ya mawasiliano ya kimataifa bila leseni ya TCRA.
Katika shitaka la pili, ilidaiwa kuwa siku na tarehe za tukio la kwanza, mshtakiwa alitoa huduma za simu za kimataifa bila kuwa na leseni ya TCRA.
Upande huo wa Jamhuri uliendelea kudai kuwa, shitaka la tatu, kati ya Januari na Novemba mwaka 2013, eneo la Kariakoo jijini Dar es Salaam, kwa nia ovu na kwa makusudi, mshtakiwa alitumia kadi za simu zenye namba 23 tofauti zisizokuwakuwa na usajili.
Wakili huyo Mwandamizi alidai katika shitaka la nne kuwa, siku na mahali pasipofahamika jijini Dar es Salaam, mshtakiwa aliingiza nchini mitambo ya elektroniki bila leseni ya TCRA.
Katika shitaka la tano, kwamba siku isiyofahamika eneo la Kariakoo, jijini mshtakiwa alisimika mitambo minne ya electroniki bila leseni ya TCRA.
Ilidaiwa katika shitaka la sita, Novemba 22,mwaka 22013 eneo la Kariakoo wilaya Ilala, jijini mshtakiwa akiwa na nia ovu na kwa makusudi, alitumia mitambo ya elektroniki ambayo ilikuwa haijathibitishwa na TCRA kutoa huduma ya mawasiliano ya kimataifa.
Katika shitaka la saba ilidaiwa kuwa, kati ya Julai mwaka 2010 na Novemba 2013, jijini Dar es Salaam, mshtakiwa akiwa hana leseni ya kumruhusu kufanya huduma za mawasiliano alichepusha simu za kimataifa na kuisababishia serikali hasara ya Sh. 6,842,880 kwa TCRA na serikali.
Mshtakiwa alikana mashitaka yote na upande wa Jamhuri ulidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika.
Hakimu Kisoka alisema mshtakiwa atakuwa nje kwa dhamana kwa kuwasilisha mahakamani fedha taslimu Sh. Milioni 3.4, wadhamini wawili wanaofanya kazi katika taasisi za kuaminika.
Mshtakiwa alishindwa kutimiza masharti hayo na alipelekwa mahabusu hadi Aprili 8, mwaka huu kesi hiyo itakapotajwa.
mtuhumiwa Nelson Onyango akiwa amepozi mahakamani akisubiri kusomewa mashitaka yake saba ya kutoa na kuchepusha mawasiliano ya kimataifa bila kibali cha TCRA. Anadaiwa kuisabishia serikali hasara ya Sh. milioni 6.8
Mtuhumiwa Onyango (mwenye tishet iliyoandikwa LEE) wakati akisindikizwa na askari. Picha na Mwene Said wa dawati la mahakamani la Globu ya Jamii
Aliyo yafanya Nelson Onyango wa Kenya hapa Tanzania, ndicho wanacho taka kufanya ndugu zetu Madiaspora wakidai Uraia wa Tanzania kwa nguvu sana!
ReplyDeleteHaya ndiyo Matunda ya Afrika ya Mashariki!
ReplyDeleteHawa jamaa jirani zetu wa EAC na hawa ndugu zetu Majuu Madiaspora wana lao jambo wanapolazimisha mambo hasa kutaka kuingia Tanzania kama inzi.
Aliyo yafanya Nelson Onyango wa Kenya hapa Tanzania, ndicho wanacho taka kufanya ndugu zetu Madiaspora wakidai Uraia wa Tanzania kwa nguvu sana!
Mkenya wa nchi jirani tu hapo ametuchambua Watanzania kama karanga kwa kuja kuendesha biashara bila Leseni Tanzania kama vile ni msituni.
ReplyDeleteJe, na ninyi ndugu zetu Madiaspora si mtatutoa damu kabisa kwa mawizi yenu ya huko Majuu tukiwapa Uraia Pacha?
Haina ata aja ya kujadili hii mada, yaani makosa ya kumwachia Mkenya afanye ujambazi ni yenu, lakini mnasingizia Madiaspora?!!. Ujinga mmfanye nyie,mnasingizia mtu mwingine. Jinyongeni tu, uraia pacha uwe, usiwe maisha ya nadunda. Poleni sana watu wenye wivu...........
ReplyDelete"Mind is a terrible thing to waste" Kafanye kazi jamani badala ya kuongea pumba humu, nyie mnaopinga diaspora. Ngoja niende zangu nikafanye kazi msije mkaniambukiza upumbavu. Bye!
ReplyDelete