Ridhiwani afanya mikutano mitano ya hadhara na miwili zaidi maalum kwa Wazee na Vijana wa Kiwangwa,maeneo ambayo mgombea wa ubunge kupitia CCM alifanya mikutano ya hadhara ni Kijiji cha Msuguru,Mwetemo,Msinune,Bago na Kiwangwa.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye ambaye pia ndio mratibu wa shughuli za kampeni za ubunge wa jimbo la Chalinze akihutubia umati wa watu waliofurika kwenye uwanja wa kata ya Kiwangwa.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akimnadi mgombea wa Ubunge kupitia CCM Ndugu Ridhiwani Kikwete kwa wananchi wa Kijiji cha Kiwangwa katika jimbo la Chalinze.
Mratibu wa Kampeni za CCM Jimbo la Chalinze Nape Nnauye wakicheza muziki kidogo pamoja na Mgombea wa Ubunge Jimbo la Chalinze kupitia CCM wakati wa kumtambulisha na kumnadi mgombea huyo kwa wapiga kura wa Kiwangwa.
Mgombea wa Ubunge Jimbo la Chalinze kupitia CCM Ridhiwani Kikwete akihutubia mamia ya watu waliofurika kwenye mkutano wa kampeni za CCM na kusisitiza tashirikiana nao bega kwa bega katika kuleta maendeleo.
Umati wa wakazi wa Kiwangwa wakimsikiliza mgombea wa ubunge jimbo la Chalinze kupitia CCM Ndugu Ridhiwani Kikwete ambapo aliwaambia wananchi hao kuwa amedhamiria kuinua wananchi wa jimbo hilo kielimu,afya,maji na namna ya kutatua tatizo la wakulima na wafugaji kuwasaidia vijana na kusisitiza kuna umuhimu wa kudumisha michezo kwa jimbo la Chalinze.
Msanii Maarufu 'Dokii' akicheza na madansa wake wakati wa mkutano wa kampeni za ubunge za CCM jimbo la Chalinze .
Vijana wa Boda Boda wakiongoza msafara wa mgombea wa ubunge CCM Ndugu Ridhiwani Kikwete kuelekea kwenye mkutano wa hadhara.
Mgombea wa Ubunge CCM Ndugu Ridhiwani Kikwete akizungumza na Bibi Tanazina Mrisho Mfaume wa kijiji cha Msinune ambapo pamoja na mengi waliyoongea pia Bibi alielezea furaha yake na kuzungumzia CCM inavyoleta maendeleo kwa wananchi wake.
Ridhiwani kila la kheri ndugu yangu.Kwa kiongozi anayehusika na eneo hili la barabara mpya ya kutoka Bagamoyo-Msata.Kunahitajika kituo cha kuuzia mafuta(fuel station) a.k.a "SHELL".Nilipita majuzi,'mkeka' safi kabisa lakini nikawa naona chupa za rangi ya pinki na chungwa hivi zimepangwa karibu kila kijiji.Mwanzo nilidhani ni juisi ya mnazi kumbe ni petriol/diesel.Kukaa na chupa za petrol majumbani ni hatari sana kwa usalama wa wananchi ingawa ni biashara inayowaingizia kipato.Nukta
ReplyDeleteDavid V
Ridhwan nakuombea kila la heri but hakikisha hawa watu wanapata matumaini mapya waondokane na hizo nyumba za makuti na visima vya maji vinavyomaliza watoto wao na pia ndoa nyingi kutetereka kutokana na wanawake kuchukua muda mwingi kutafuta maji
ReplyDelete