Mgombea Ubunge katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze kwa tiketi ya CCM,Ridhiwani Jakaya Kikwete (kushoto) akiwa na Bw. Geofrey Nestory pamoja na Mkewe,Renata Pascal ambao ni Wazazi wa Watoto wawili,Jesca Geofrey (5) na Redempta Geofrey (2) waliopoteza maisha hivi karibuni kwa kutumbukia kwenye kisima cha maji,wakati alipofika Nyumbani kwa wazazi hao ambao ni Wakazi wa Kijiji cha Msinune,Kata ya Kiwangwa leo Machi 22,2014 kuhani msiba wa Watoto hao.Wazazi hao walimueleza Ndg. Ridhiwani Kikwete kuwa walibaini kupotea kwa watoto hao mnamo tarehe 18 Machi wakati wa jioni baada ya kuona hawajarudi nyumbani,hivyo walianza kuwatafuta na kubaini kuwa walipoteza maisha baada kuingia kwenye kisima hicho cha maji.Watoto hao walizikwa siku ya pili yake tarehe 19 Machi,Shambani kwao.
 Mgombea Ubunge katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze kwa tiketi ya CCM,Ridhiwani Jakaya Kikwete akiwa amesimama kutoa pole kwa Wazazi wa Watoto hao pamoja na Waombolezaji Wengine waliokuwepo msibani hapo,kwenye Kijiji cha Msinune,Kata ya Kiwangwa leo Machi 22,2014.
Meneja wa Kampeni za CCM katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze,Ndg. Steven Kazidi akitoa pole kwa niaba ya CCM kwa Watoto wawili,Jesca Geofrey (5) na Redempta Geofrey (2) waliopoteza maisha hivi karibuni kwa kutumbukia kwenye kisima cha maji,wakati walipofika Nyumbani kwa Wazazi hao kuhani msiba huo leo Machi 22,2014.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Inshallah muheshimiwa Ridhwan utashinda na kuwasaidia hawa wananchi. You will satisfy their needs.RIDHWAN in Arabic means "satisfaction" its yor destiny, and remember this family and get rid of that kisima cha maji na waletee bomba la maji
    ibrahim.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...