Na Tiganya Vincent-Dodoma 
 Mwenyekiti wa Wabunge Wanawake wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Anna Abdallah ametoa wito kwa wajumbe wanawake wa Bunge Maalum la Katiba kufanya kazi kwa ushirikiano katika kuhakikisha kuwa wanaweka maslahi ya mwanamke mbele katika uandishi wa Katiba mpya na sio vinginevyo. 
 Mwenyekiti huyo ametoa kauli hiyo leo mjini Dodoma wakati anafungua semina ya siku moja ya wajumbe wanawake wa Bunge Maalum la Katiba iliyoandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake nchini (TAMWA) kwa lengo la kuwaelimisha juu ya kuwepo na haja ya kuwepo na vipengele vinavyotetea haki za wanawake na watoto katika masuala mbalimbali. 
 Alisema kuwa wajumbe hao wanawanawake wanapaswa kuweka kando tofauti zao za kivyama, kiitikadi na kiimani na kuhakikisha kuwa haki za msingi zinaweka katika Katiba mpya itakayotunga ili kujenga usawa wa kijinisia katika masuala mbalimbali hapa nchini. 
Mhe Anna Abdallah aliongeza kuwa ni vema wajumbe hao wakatumia fursa hiyo wliyoipata ya kuingia katika Bunge hilo maalum katika kuhakikisha kuwa vipengelea vinavyolinda haki za Wanawake na watoto na kupigania uwepo wa usawa wa asilimia hamisni kwa hamisi katika masuala mbalimbali. 
 Aidha aliongeza kuwa ni jukumu la wanawake wote walioko katika madaraka kuwatetea wanawake wengine ambao wako nje na hata kuwahamasisha kwa kuwapa moyo wa kuingia katika siasa na kuwania madaraka mbalimbali badala ya kuwakatisha tama. 
 Akitoa mada katika Semina hiyo Mkurugenzi Mttendaji wa TAMWA Valerie Msoka alisema kuwa ni vema wajumbe hao wakapigani wazi umri wa mtoto uwekwe wazi na pia umri wa kuweza kuoa na kuolewa. 
 Aliongeza kuwa mambo mengine ni pamoja na kuweka vipengele vinavyopinga ukatiili wa kijinsia kama vile kupinga ndoa za utotoni, ukeketaji , kulazimishwa biasha ya mapenzi na ubakaji. 
 Naye Makamu Chansela wa Chuo Kikuu cha Hubert Kairuki Profesa Esther Daniel alisema kuwa suala la uzazi salama ni muhimu likazingatiwa katika uandishi wa Katiba mpya ili kuzuia mimba za utotoni na vifo vinavyotokana na uzazi.
 Mwenyekiti  wa Wabunge wanawake Anna Abdallah (kulia) akifungua semina ya Wabunge wanawake wa Bunge Maalum la Katiba leo mjini Dodoma uliokuwa ukijadiliana juu ya umuhimu wa kuwekwa kwa umri wa mtoto katika Katiba mpya  na umri unatakiwa kuolewa na kuoa na masuala ya uzazi salama.  Kushoto ni Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe AngelahKairuki.
 Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe Angelah Kairuki akitoa maoni yake leo mjini Dodoma wakati wa Mkutano wa Wabunge wanawake wa Bunge Maalum la Katiba uliondaliwa na Chama cha Waandishi  wanawake Tanzania (TAMWA) juu ya kuwaelimisha masuala mbalimbali ya kuzingatia wakati wa utungaji wa Katiba mpya ikiwemo uzazi salama na kutoa ufafanuzijuu ya umri wa mtoto.
 Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA Valerie Msoka akitoa mada kwenye semina iliyoandaliwa na TAMWA kwa ajili ya wabunge wanawake wa  Bunge Maalum la Katiba  leo mjini Dodoma juu ya kuingiza vipengele ambavyo vitasaidia kutokomeza ukatilii wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto wakati wa uandishi wa Katiba mpya.  
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Margareth Sita akitoa maoni yake leo mjini Dodoma wakati wa Mkutano wa Wabunge wanawake wa Bunge Maalum la Katiba uliondaliwa na Chama cha Waandishi wanawake Tanzania (TAMWA) juu ya kuwaelimisha masuala mbalimbali ya kuzingatia wakati wa utungaji wa Katiba mpya ikiwemo uzazi salama na kutoa ufafanuzijuu ya umri wa mtoto.
 Mjumbe wa Bunge la Katiba ambaye pia  Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Ummy Mwalimu akitoa maoni yake leo mjini Dodoma wakati wa Mkutano wa Wabunge wanawake wa Bunge Maalum la Katiba uliondaliwa na Chama cha Waandishi  wanawake Tanzania (TAMWA) juu ya kuwaelimisha masuala mbalimbali ya kuzingatia wakati wa utungaji wa Katiba mpya ikiwemo uzazi salama na kutoa ufafanuzijuu ya umri wa mtoto. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...