THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE
OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
Telephone: 255-22-2114512, 2116898
E-mail: ikulumawasiliano@yahoo.com
Fax: 255-22-2113425 |
|
PRESIDENT’S OFFICE,
THE STATE HOUSE,
P.O. BOX 9120,
DAR
ES SALAAM.
Tanzania.
|
TAARIFA KWA VYOMBO VYA
HABARI
SALAMU ZA RAMBIRAMBI ZA RAIS
WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHESHIMIWA DKT. JAKAYA MRISHO KIKWETE
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia Salamu za Rambirambi Waziri wa
Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa
na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe.
Hawa A. Ghasia kufuatia kifo cha Mkuu wa Mkoa wa Mara, Mhe. John Gabriel Tuppa,
aliyefariki leo tarehe 25 Machi, 2014 katika Hospitali ya Wilaya ya Tarime.
Pokea rambirambi zangu za dhati na masikitiko makubwa kufuatia kifo cha
Mhe. John Gabriel Tuppa. Ni huzuni kubwa na pigo kwa Serikali na hasa kwa
Watendaji wenzake mkoani Mara ambao alikuwa akifanya nao kazi. Marehemu
John Gabriel Tuppa amefariki leo tarehe 25 Machi,2014 katika Hospitali ya
Wilaya ya Tarime.
Rais pia amemwomba Mhe. Ghasia amfikishie
salamu za pole kwa Mke wa
Marehemu,Watoto na Familia ya Marehemu kwa kuondokewa na kipenzi chao. Rais
amesema, anaelewa machungu wanayoyapitia katika kipindi hiki kigumu kwani
wamepoteza nguzo imara waliyokuwa wakiitegemea katika maisha yao.
“Hakika tumempoteza kiongozi mchapakazi
ambaye amekuwa akijituma na kuwatumikia
Wananchi wake hadi dakika za mwisho za uhai wake. Pengo aliloliacha Marehemu Tupa haliwezi
kuzibika kamwe lakini hatuna budi kumwombea kwa Mwenyezi Mungu kuipumzisha roho
ya Marehemu mahali pema peponi” Amina.
Taratibu na maandalizi ya mazishi zinafanywa
kwa ushirikiano wa Familia, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mara na Ofisi ya Waziri
Mkuu TAMISEMI.
Marehemu Tupa alizaliwa tarehe 01 Januari,
1950 na katika enzi za uhai wake amewahi kuongoza Wilaya za Chunya, Mwanga, Bukoba, Muleba na Dodoma
kabla ya kuteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara Mwaka 2011. Ameacha Mke na watoto
watano.
Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
25 Machi,2014
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...