Pichani kati ni Meneja wa bia ya Serengeti Bw Rodney Rugambo akizungumza na Waandishi wa habari (hawapo pichani),mapema leo jijini dar kuhusiana na mshidi aliyejishindia tiketi ya kwanza ya kwenda nchini Brazili
Meneja wa bia ya Serengeti Bw Rodney Rugambo akizungumza na mshidi huyo kwa njia ya simu ya kiganjani.
SBL YACHEZESHA DROO YA NNE YA PROMOSHENI YA WINDA SAFARI YA BRAZILI NA SERENGETI YAENDELEA .
Hatimaye mshindi wa kwanza wa tiketi ya kwenda Brazili kupitia bia ya Serengeti apatikana.
Baada ya kusubiri kwa kipindi cha wiki 3 hatimaye mshindi wa kwanza wa tiketi ya kwenda Brazili kupitia promosheni ya 3 Winda Safari ya Brazili na Serengeti amepatikana katika droo ya nne ya promosheni hiyo. Katika droo hiyo pia wamepatikana washindi wawili wa simu aina ya Samsung galaxy tab, pamoja na washindi hao wa droo pia kuna washindi waliojipatia zawadi za papo hapo kama bia za bure, fedha taslimu pamoja na ving’amuzi.
Droo hiyo imechezeshwa leo asubuhi katika ofisi za Kampuni ya Bia ya Serengeti huku ikishuhudiwa na waandishi wa habari, maofisa kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, PWC na push mobile media. Promosheni hiyo bado ina wiki 8 mbele hadi kumalizika na ndani yake bado droo kubwa 2 za kujishindia tiketi za kwenda Brazili.
Akiongea kwa furaha iliyopita kifani kwa njia ya simu mshindi wa kwanza wa tiketi ya kwenda Brazil Deusdedit Kahwa kutoka Mbezi, Dares Salaam alisema alipata mshangao mkubwa sana kwa kuwa hakutarajia kupata bahati hii ya kuwa mshindi wa tiketi na alishiriki promosheni hii baada ya kuona matangazo yake kwenye televisheni. Aliishukuru Kampuni ya Bia ya Serengeti kwa kumpa fursa hiyo kubwa katika maisha yake na kuipongeza kwa kuwajali wateja wake kwa kuwapa zawadi mbalimali zinogusa maisha yao.
“nimefurahi sana na ninajiona mwenye bahati sana kwa kushinda zawadi hii kubwa, hii ni mara ya kwanza kushinda zawadi katika promosheni hii na nimepata zawadi kubwa sana na itakuwa ni mara yangu ya kwanza kutoka nje ya nchi, nawashukuru sana Serengeti kwa kutujali wateja wao” alimalizia Deusdedit.
Meneja wa bia ya Serengeti Bw Rodney Rugambo alisema kuwa promosheni hiyo ipo wazi kwa wanywaji wote wa bia ya Serengeti, na mpaka sasa kumekuwa na washindi Zaidi ya 50000 waliojishindia bia za bure na pia zaidi ya washindi 2000 wa fedha taslimu kiasi cha shilingi 5000 na 10,000. Washindi waliojishindia simu za Samsung tab katika droo ya leo ni Deo Msofe kutoka Kiboroloni, Moshi na Jeremiah Ndelekwa kutoka Arusha. Pia wamepatikana washindi watano (5) wa ving’amuzi ambao wote kwa pamoja watakabidhwa zawadi zao katika sherehe maalum.
Nae Meneja Masoko wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Bw Allan Chonjo alisema “promosheni ya Winda Safari ya Brazil na Serengeti bado inaendelea na tunapenda kuwakumbusha wateja wetu kuwa hii ndio tiketi ya kwanza bado kuna tiketi nyingine na zawadi nyingine nyingi zaidi, unaweza kufuatilia kupitia ukurasa wetu wa facebook www.facebook.com/serengetipremiumlager kwa taarifa zaidi. Napenda kuwashukuru wateja wetu kwa kuendelea kutumia bidhaa zetu na sisi tunawaahidi kuendelea kuwapa bidhaa zilizo bora na zenye viwango na ubora wa hali ya juu”
Kunywa kistaarabu. Washiriki wanatakiwa kuwa na umri unaozidi miaka 18. Vigezo na masharti kuzingatiwa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...