Na Asteria Muhozya, Bangkok,
Kutokana na kuwa na hazina kubwa ya madini ya aina mbalimbali hususani madini ya vito na usonara tofauti na nchi nyingi za Kiafrika, yakiwemo madini ya Tanzanite, Shirikisho la madini ya vito na usonara la Thailand, limehaidi kuisaidia Tanzania kuikuza sekta hiyo, katika nyanja za kibiashara na kiuchumi ili kuifanya Tanzania kuwa, kitivo kikubwa cha madini barani Afrika, huku ikianzia na kuboresha maonesho ya kimataifa ya madini ya vito na usonara ya Arusha yanayofanyika kila mwaka.
Aidha, nia ya shirikikisho hilo imetokana na uwepo wa makampuni mengi ya wafanyabiashara wa Thailand kupenda madini yanayotoka Tanzania ikiwa pia ushirikiano mzuri uliopo kati ya Tanzania na Thailand.
Hayo yamesemwa kwa nyakati tofauti na Viongozi wa Shirikisho la madini ya vito na usonara Thailand na kiongozi kutoka Idara ya Ukuzaji Biashara ya Kimataifa katika Wizara ya Biashara ya Thailand.
“Tunataka kuisaidia Tanzania kutengeneza fursa nyingi zaidi za kibiashara katika tasnia hii. Tanzania ina kila sababu ya kufanikiwa katika hili, kuna madini mengi na bora ya kuifanya kuwa kituo kikubwa cha madini Afrika”. Amesema Tom Broke, Makamu wa Rais wa Shirikisho la madini ya Vito na usonara Thailand.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Idara ya Ukuzaji Biashara ya Kimataifa katika Wizara ya Biashara ya Thailand, Bibi Nuntawan Sakuntanaga, ambaye amelitembelea banda la Tanzania na kufurahishwa na aina za madini zilizowasilishwa, amehaidi kuboresha maonesho hayo ili kuziwezesha nchi zenye hazina kubwa kama Tanzania kuweza kushiriki maonesho hayo kwa kiwango kikubwa.
“Tanzania inashiriki katika maonesho haya kwa mara ya kwanza, tunataka kuwasaidia katika hili, ili muweze kujenga mtandao mkubwa zaidi wa kibiashara kwasababu mna kila sababu ya kufanikiwa kutokana na umuhimu wenu katika sekta hii. Sisi sote tunawahitaji ninyi.” Amesema Bibi. Sakuntanaga.
Hivyo, amewataka wafanyabiashara wa Kitanzania kujenga mtandao wa kibiashara na wadau wengine duniani kutokana na ubora wa madini yanayopatikana nchini.
Wakati huo huo, Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara wa Madini Tanzania, (TAMIDA) Bw. Sam Mollel, amewaomba viongozi wa Shirikisho hilo kuhakikisha kuwa wanaboresha mazingira ya kibiashara kati ya Tanzania na Thailand ili kuwawezesha wafanyabiashara wa madini kushiriki kwa wingi na kuleta bidhaa nyingi zaidi katika maonesho mengine nchini humo ikiwemo kufanya biashara na Thailand.
Kwa upande wake kamishna Msaidizi Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Hamis Komba, ameeleza kuwa, jambo hilo ni fursa kubwa kwa Tanzania na wadau wa madini nchini ambayo wanahitaji kuitumia kikamilifu kutokana na nafasi kubwa ambayo Tanzania imepewa katika maonesho hayo na utayari wa nchi ya Thailand kutaka kushirikiana na Serikali na wafanyabiashara wa madini wa Tanzania.
Ameongeza kuwa, maonesho ya madini ya Arusha ni fursa nyingine kwa Tanzania kutokana kuwa nchi pekee katika ukanda wa Afrika, ambayo inafanya maonesho ya vito vya madini na usonara, Afrika.
“Tumejidhatiti kujifunza kutoka kwao na tumefarijika kuona namna wafanyabiashara mbalimbali wanavyothamini madini yetu na maonesho yetu ya Arusha. Hiyo ni hatua ya kuifanya Tanzania kuwa kitovu cha madini”. Amesema Kamishna Komba.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Idara ya Ukuzaji Biashara ya
Kimataifa katika Wizara ya Biashara ya Thailand, Bibi Nuntawan Sakuntanaga,
akiangalia madini aina ya Tanzanite, alipotembelea banda la Tanzania. Wa kwanza
kulia ni Kamishna Msaidizi wa Madini, Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi
Hamis Komba, wa tatu kulia ni Makam wa
Rais wa Shirikisho la madini ya vito na usonara, Thailand Bw. Tom Broke,
wengine wanaoshuhudia ni wawakilishi wa Tanzania katika maonesho hayo.
Mkurugenzi Mtendaji
Idara ya Ukuzaji Biashara ya Kimataifa katika Wizara ya Biashara ya Thailand, Bibi
Nuntawan Sakuntanaga, katika picha ya pamoja na ujumbe wa Tanzania katika
maonesho ya 53 ya ‘Bangkok Gems and Jewelry Fair’’.
Wafanyabiashara wa
madini kutoka nchi mbalimbali wakiangalia madini ya almasi katika banda la
Tanzania. Wanaohushudia ni Bib.Teddy Goliama kutoka idara ya uthamini madini ya
almas wizara ya nishati na madini na wa pili ni Bw. Gregory Kibusi mchimbaji wa
madini.
Asante sana Mapidnuzi ya biashara ya Dunia kwa kutoa 'Certificates of Origin' kwa kila bidhaa ya dunia kwa nchi inakotoka.
ReplyDeleteHawa jamaa Thailand wametumia akili sana kwa sababu wamesha tumia sana madini ya Tanzania kujinufaisha Kibiashara na Kiuchumi.
Na sasa kwa kuwa hakuna bidhaa ya nchi yeyote ya dunia unaweza kuiiuza nje kwenye masoko ya dunia bila kuwa na 'Certificate of origin' inayotolewa na kuratibiwa na WTO 'World Trade Organization' ni lazima itafahamika imetokea wapi asili yake.
Hivyo baada ya Usajili wa Dirisha Dogo kufungwa Thailand kwa Madini ya Tanzania, wameona washirikiane na sisi Tanzania wenye 'origin' ya madini hayo kitu ambacho ni akili ya ziada kuendelea na bishara lakini kwa njia halali kwa sasa!!!
Kuna kila sababu ya sisi kuanza kunufaika na mali zetu ikiwemo madini!
ReplyDeleteNi vile huwezi chukua rasilimali ya nchi ingine ukauza kwako kutokana na mtindo mpya wa Biashara ya dunia wa e-CO 'Electronic-Certificate of origin' inashindikana.
Jirani zetu Kenya wangekuwa na akili wangefanya kama wanavyo fanya Thailand badala ya kutuchukia!
ReplyDeleteKenya imekuwa ikiuza madini na mali nyingi za Tanzania miaka nenda miaka rudi lakini kutokana na mabadiliko haya ya bishara ya dunia kwa mujibu wa WTO (World Trade Organiztion) na WTC (World Trade Center) na UNCTAD ndio tunashuhudia Soko Kubwa la Madini la Afrika ya Mashariki limefunguliwa Arusha-Tanzania !