N a Magreth Kinabo ,Dodoma
Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba,Mhe. Samwel Sitta leo (jana), ametangaza majina ya wenyeviti na makamu wenyeviti wa Kamati za bunge hilo.
 Majina hayo yametangazwa na Mwenyekiti huyo  baada ya uchaguzi wa viiongozi hao uliofanyika  (jana) Machi 24 , mwaka  2014 mjini  Dodoma .
Mwenyekiti ametangaza majina haya baada ya kuunda kamati hizo  jana kwa mujibu wa kanuni ya 54 (1) ya kanuni za Bunge Maalum za Mwaka 2014 ambazo zimetungwa chini ya kifungu cha 26 (1) cha sheria ya Mabadiliko ya Katiba sura ya 83, ambazo zinataja kuundwa kwa kamati 12 za Bunge Maalum.  
Wenyeviti na makamu wenyeviti waliochaguliwa katika kamati hizo ni pamoja na  Kamati  ya Uandishi ambayo Mwenyekiti   amechaguliwa Mhe. Andrew Chenge, Makamu wake ni Mgeni Hassan Juma. Kamati ya Kanuni Mwenyekiti ni Pandu Ameri Kificho, Makamu wake ni Dkt. Susan Kolimba. Kamati Na. 1 Mwenyekiti ni  Ummy Ally Mwalimu, na Makamu wake ni  Prof. Makame  Mbalawa
Wengine waliochaguliwa  katika Kamati Na. 2  ni  Shamsi Vuai Nahodha ambapo Makamu wake ni  Shamsa Mwangunga, Kamati Na. 3 Mwenyekiti ni  Dkt. Francis Michael, Makamu wake ni Fatma Mussa Juma.
Mhe. Sitta alisema waliochaguliwa katika Kamati Na. 4 Mwenyekiti ni  Christopher  Ole-Sendeka, Makamu wake ni  Dkt. Sira Ubwa Mamboya, Kamati Na. 5 Mwenyekiti ni  Hamad Rashid Mohamed Makamu wake ni  Assumpter  Mshama.
Waliochaguliwa katika Kamati Na. 6 Mwenyekiti ni Stephen Wassira na Makamu wake ni  Dkt. Maua Daftari, Kamati Na. 7  Mwenyekiti  Brig. Hassan Ngwilizi  ,Makamu wake  Waride BakariJabu, Kamati Na. 8 Mwenyekiti   ni Job Ndugai,Makamu wake ni Biubwa Yahya Othman.
Hali kadharika Kamati Na. 9 Mwenyekiti ni Kidawa Hamidi Saleh, Makamu wake Wiliam  Ngeleja, Kamati Na. 10 Mwenyekiti ni Anna  Abdallah, Makamu wake ni Salmin Awadh Salmin, Kamati Na. 11 Mwenyekiti ni  Anne  Malecela, Makamu wake  Hamad  Masauni na Kamati Na. 12 Mwenyekiti  niwake  Paul  Kimiti na Makamu wake ni  Thuwaybah E. Kisasi.
Aidha, kwa uchaguzi huo, Mhe. Sitta  alitangaza wajumbe wa Kamati ya  Uongozi ya Bunge Maalum la Katiba ambao  ni wenyekiti wote wa kamati hizo wakiwemo wajumbe wengine watano aliowateua kwa mujibu wa Kanuni.
Wajumbe hao walioteuliwa na Sitta kuingia katika kamati hiyo ni pamoja na Fakharia Khamisi Shomari, Mary Chatanda, Profesa Ibrahim Lipumba, Amon Mpanju na Hamoud Abuu Juma. Hata hivyo pamoja na majina hayo kutangazwa Profesa Lipumba alisimama na kujitoa katika nafasi hiyo hivyo kufanya nafasi za uteuzi kuwa nne badala ya Tano .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. Jamani, it's now 8 weeks and these people have done nothing Bali kuchaguana, do they really know what they are supposed to do? God bless bongoland12

    ReplyDelete
  2. Ulaji halali wa kodi zetu

    ReplyDelete
  3. Yehhhh,eight weeks but they know what they are doing.They want to do everything efficiently and effectively,u wait and c. Or do u want them to rush ?

    ReplyDelete
  4. muda umekuwa unaenda tu. Hebu wajumbe muwe kikazi zaidi

    ReplyDelete
  5. And they are loving it, they will be there till Xmas

    ReplyDelete
  6. mtu akiwa ulaya kiswahili anajifanya hakijui

    ReplyDelete
  7. Bora niendelee kupiga box,hilo li nchi lilishashindikana..yaani katiba dili!!wanakaa masaa 3 then wanahairisha kikao ni ulaji kwa kwenda mbele hamna lolote wanalofanya hapo..ndo maana hata hio dual citizenship siitaki hata kuisikia ya nini kwanza kuwa raia kwenye nchi ya wavivu??to hell with uraia pacha!!

    ReplyDelete
  8. The time they have been given by the constitutional law review is still in intact, please let give them time to make sure they do what we send them there to do. All these are procedures that are necessary in any true democracy. If they rush, the outcome will be a burden to all of us.

    ReplyDelete
  9. Anonymous #6 nakubaliana na wewe lakini mbona hata viongozi wetu wanaongea lugha hiyo hiyo kama ya jamaa?!!. Mfano, mkuu Kikwete kwenye hotuba ya katiba ameongea Kiingereza kibao lakini sikusikia mtu analalamika kitu humu au kwa vile ni jamaa wa Ughaibuni, chochote wafanyacho ni kosa?. Mkuu#7 umeniacha mbavu sina. Lakini lazima tudai haki yetu, itapatikana tu.
    *Mmbongo Chiberia*

    ReplyDelete
  10. I'm a USA citizen And happy than never before, don't need that dual citizenship, being a Tanzanian will make me to continue paying attention to a country that is always wanna stand to a status quo, what was the intention of writing a new constitution if the leaders Didn't wanna change anything in the first place?a lot of money was wasted collecting people's opinions a lover the country and now the opinion is viewed As a bad idea, so why would they spend all the money and wasted time and now gathered to debate on the draft they don't want. WASTING TIME AND TAX PAYERS MONEY ......Michuzi it's my opinion and I express freedom of speech so don't dump my comment

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...