Kama mlivyofahamishwa awali Mtanzania mwenzetu Mama Lulu John Maro Mwaluko (pichani) amefariki dunia asubuhi ya siku ya Ijumaa tarehe 7 Machi 2014.
Mama Mwaluko alikuwa akikaa Queens, New York, na alishawahi kuwa mwalimu na alifundisha high school hapa New York.
Mama Mwaluko alifariki baada ya kuugua ugonjwa wa saratani yaani kansa. Alikuwa akitibiwa huko katika hospitali ya Calvary huko Bronx, New York.
Mama Mwaluko alikuwa akikaa Queens, New York, na alishawahi kuwa mwalimu na alifundisha high school hapa New York.
Mama Mwaluko alifariki baada ya kuugua ugonjwa wa saratani yaani kansa. Alikuwa akitibiwa huko katika hospitali ya Calvary huko Bronx, New York.
Michango yenu kwa ajili ya kufanikisha shughuli za msiba huu itumwe kwenye akaunti ifuatayo:
Bank: Citibank
Routing Number: 021000089
Account Number: 02472079
Bank Address: Citibank, Jamaica 89-50 164th St, Jamaica, NY 11432.
Jina la Account: Nanna Mwaluko na Helen Mwaluko.
Mama Mwaluko alishawahi kukaa na Marehemu mumewe China na Marekani kama Wanadiplomasia na alishastaafu kufundisha mwaka 2012 na kabla ya kufariki alikuwa mbioni kurejea Tanzania.
Mama Mwaluko atakumbukwa na familia yake kama mama, dada, shangazi, mwalimu, mcha Mungu na mama mwenye busara. Katika kuomboleza msiba wa Mama Mwaluko, Watanzania wote tunaombwa kuifariji familia yake na ndugu zake kwa kujumuika nao katika sala na michango katika wakati huu mgumu wa maombolezo.
Mnaweza kuwasiliana na Emma Kasiga kwa simu namba 612-229-4050 na Nanna Mwaluko kwa simu namba 347-693-6129 na Camelot Funeral Home kwa simu namba 914-664-8500. Taarifa zaidi za msiba huu zitafuata baadae.
Siku ya Jumatano itakuwa ni siku ya kuaga mwili wa Marehemu kuanzia saa tisa na nusu hadi saa mbili za usiku pale Camelot Funeral Home. Anwani ni:
Camelot Funeral Home,
174 Stephens Avenue,
Mount Vernon,
New York, 10550.
Wote mnaombwa kufika kumuaga
Mama Lulu John Maro Mwaluko na kuifajiri familia yake.
Imetolewa na Uongozi - Jumuiya ya Watanzania New York.
Mwenyezi Mungu aiweke roho ya
Marehemu mahali pema peponi.
Amina.
R.I.P mama Mwaluko. Umetutangulia tu sote ni waja wake muumba.
ReplyDelete