Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) inatarajia kurejea nchini kesho (Machi 7 mwaka huu) saa 12.45 jioni kutoka Windhoek, Namibia kwenye mechi ya kirafiki ya kalenda ya FIFA.

Taifa Stars ambayo katika mechi hiyo dhidi ya Namibia (Brave Warriors) ilitoka sare ya bao 1-1 itatua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) saa 8.15 mchana kwa ndege ya South Africa Airways.

Timu inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager baada ya kuwasili itakwenda hoteli ya Accomondia kwa ajili ya chakula cha mchana na baadaye kuvunja rasmi kambi yake.

Boniface Wambura Mgoyo
Media and Communications Officer

Tanzania Football Federation (TFF)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Hongera Taifa Stars na benchi la utaalamu matokeo 1-1 yanakubalika katika mchezo wa kirafiki muhimu benchi la utaalamu wapatiwe uwezo wa kujiwakilisha katika michezo ya ligi kusaka vipaji vipya vya kuungana na wazoefu kupata kikosi
    kitakachotuwakilisha tusipoteze muda kusaka mwalimu tunaweza kuanzia na benchi la uteuzi hadi mwalimu mpya na CV ya uhakika.
    Mikidadi-Denmark

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...