Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) lilifikia makubaliano na kampuni ya Adidas kupitia msaada wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) kupatiwa vifaa vya michezo.

Kufuatia makubaliano hayo TFF tulipatiwa vifaa kadhaa vya adiads kwa ajili ya timu ya Taifa ya wakubwa (Taifa Stars). Vifaa hivyo zikiwemo jezi tulianza kuvitumia kwenye mechi ya kirafiki dhidi ya Namibia iliyochezwa Machi 5 mwaka huu jijini Windhoek kama inavyoonekana pichani.

Vifaa hivyo zikiwemo jezi vitaendelea kutumiwa na Taifa Stars hadi hapo utaratibu mpya wa jezi za timu ya Taifa utakapokamilika.

TFF tunaishukuru kampuni ya Adidas ambao ni washirika wa CAF na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) kwa miaka mingi kwa mchango wao huu wa kuendeleza mpira wa miguu nchini.

Boniface Wambura Mgoyo
Media and Communications Officer
Tanzania Football Federation (TFF)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Safi sana TFF kwa kuliona hilo.Vijana "walitokelezea" sana juzi VS Namibia:Ubora wa jezi unaonekana hata kwenye picha.Zile za awali hazikuwa nzuri sana kwa mtazamo wangu na hasa zile bukta zikiloa jasho zinakuwa kama.......!!

    David V

    ReplyDelete
  2. lakini bado tutafungwa tuu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...