Meneja wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Kanda ya kaskazini,Salvator Rweyemamu (kulia) akimkabidhi mkataba wa kukabidhiana majengo ya TBL yaliyopo Moshi, kwa Katibu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania
(KKKT), Dayosisi Kanda ya Kaskazini, Julius Mosi, katika hafla iliyofanyika mwishoni mwa wiki Moshi, mkoani Kilimanjaro. Majengo hayo yatakayotumika kwa ajili ya Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Stephano
SMMUCO) yalikuwa ya Kiwanda cha Bia cha Kibo kilichonunuliwa na TBL.
Katibu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi Kanda ya Kaskazini, Julius Mosi akikabidhi mkataba kwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Stephano (SMMUCO) Prof,Arnod Temu kwa ajili ya
kutmiwa na chuo hicho chini ya dayosisi hiyo iliyokabidhiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) katika hafla iliyofanyika mwishoni mwa wiki Moshi, mkoani Kilimanjaro.Awali majengo hayo yalikuwa ya Kiwanda cha
Bia cha Kibo kilichonunuliwa na TBL.
Baadhi ya majengo yaliyokabidhiwa
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...