Picha inayoonesha moja ya mashimo yaliyochorongwa katika Bonde la Engaruka Wilayani Monduli, Mkoa wa Arusha kuthibitisha uwepo wa hazina kubwa ya magadi soda. Hii ilidhihirishwa mbele ya Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Dkt. Philip Mpango aliyeongoza timu ya wakaguzi wa miradi ya maendeleo kutoka katika ofisi yake (hawapo pichani).
Moja ya Shimo la magadi soda katika Bonde la Engaruka.
Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Dkt. Philip Mpango (wa kwanza kushoto) akionja maji ya magadi soda yaliyotoka katika moja ya shimo lilichorongwa katika bonde la Engaruka alipoongoza timu ya wakaguzi wa miradi ya maendeleo kutoka Tume ya Mipango. Anayewamiminia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC), Bw. Gideon Nasari.
Timu ya wakaguzi wa miradi ya maendeleo kutoka Tume ya Mipango wakijaziwa maji ya magadi soda katika chupa za maji ya kunywa walipotembelea bonde la Engaruka ambako kuna hazina kubwa ya magadi soda.
Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Dkt. Philip Mpango akitazama (admires) kipande cha magadi soda katika eneo la Ziwa Natron Wilaya ya Ngorongoro Mkoa wa Arusha alipoongoza timu ya wakaguzi wa miradi ya maendeleo kutoka katika ofisi yake. Pamoja naye ni watoto wa kimasai waliokuwa wakiuza vipande hivyo vya magadi soda.Picha na Joyce Mkinga.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Thank you for visiting us, we look forward to seeing you again soon

    ReplyDelete
  2. mmmh kwanini wanakunywa hayo maji ya magadi? Magadi ni chumvi sasa mnakunywa maji ya chumvi? Halafu ndio yametoka chini huwezi jua uchafu wa huko ndio mwanzo wa magonjwa.

    ReplyDelete
  3. Wanavyoshangaa utazani ndio kwanza wamefika Tanzania!

    ReplyDelete
  4. Naomba wadau muniambie magadi soda kwa neno la kitaalam ni nini?

    ReplyDelete
  5. Aliyetaka jina la kitaalamu la magadi ni Bicarbonate soda

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...