Awali mabunda haya yalivyokutwa katika jumba la Zungu la Unga  lililovamiwa na vikosi maalumu huko Mexico yalikadiriwa kuwa ni dola bilioni 18 za Kimarekani. Baada ya kuhesabiwa ikakutwa ni zaidi ya dola bilioni  22. Hii inadhihirisha jinsi biashara ya 'Sembe' ilivyo na changamoto kubwa kwani kwa kiasi hicho mwenyewe anaweza kununua chochote ama mtu yeyote na kufanya atakalo. Lakini pamoja na hayo vikosi vya kupiga vita biashara hii haramu vinaendelea na jitihada zao kupambana nao usiku na mchana, kwa mafanikio kama haya...


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Joachim Guzman also known as The Short which means "El Chapo" in spanish

    ReplyDelete
  2. hapa nilipo nafikiria jinsi hayo mapesa yanavyoweza kuibadilisha tanzania kuwa kama dubai endapo tungezipata na kutumia vizuri

    ReplyDelete
  3. This chap is a collector of money. He must have set himself a target to fill the room up. Wewe mdau wa kwanza, unamjuaje Joachim Guzman???? Pass contact details please. Animalizie kujenga kabanda kangu pale Mswiswi.

    ReplyDelete
  4. Its illegal money,ok,
    But that does not stop me.......
    Mate yananidondoka.

    ReplyDelete
  5. USD 22 Billion ?

    Si mchezo, kazi tunayo.

    Hiyo si uwezo wa Serikali kamili?

    Ndio maana jamaa Guzman alikutwa akiwa na 'Assault Rifle' aina ya Bunduki ya Kivita ya Marekani ambayo huwezi kuipata bila ruhusa ama kupewa na Jeshi na Serikali ya Marekani!

    Alishindwa kuitumia bunduki hiyo 'Assault Rifle' alipozingirwa na Majeshi ya Vikosi Kazi vya Sembe vya Mexico na Marekani kwa pamoja ktk Operesheni ya kumkamata.

    Wazee wanasema ktk Operesheni walipata tip kuwa yupo Mjengoni kwake nyumbani, wakazama jamaa machale akala kona kwa kupitia ktk Bafu la Dimbwi la kuogea 'bath tub' ambalo amelitengeneza maalumu likiwa linajazwa maji muda wote na likiwa na njia ya shimo ya kupitia chini kwa chini na kutokea nje.

    Wanazema alishakoswa mara kama 3 au zaidi akiitumia njia hiyo ya Bafu lake kuwatoka Wazee lakini safari hii baada ya kuwatoka wakatumia Tekinolojia ya 'wire taping' yaani walifuatilia mawimbi ya mawasiliano ya simu yake wakagundua yupo ktk Hoteli moja ya Ufukweni ndipo wakamfuata na wakamrukia wakamkuta na mkewe wakamweka mkononi!

    Lakini kutokana na Mzigo wa Noti zake USD 22 Billion ameweza kuikamata bunduki hiyo adimu ya Kivita ya Kimarekani.

    Sasa hapo ndio tutatambua jinsi Vita dhidi ya Biashara ya Sembe na Matajiri wake waliokuwa vizuri kifedha ilivyo kuwa ngumu!!!

    ReplyDelete
  6. Madhara mengine ya 'Sembe' ktk Uchumi ni kuwa kama tunavyoona idadi kubwa ya fedha USD 18 Bilioni zipo chumbani kwa mtu na mkewe (inavyoonekana chuma hata rangi ya ukutani ya maana hakina) zikiwa hazitumiki ktk mzunguko wa Mitaji, Biashara na Uwekezaji kukuza Ajira na kuchuma Kodi kwa Faida ya bishaara na kujenga Uchumi.

    Haiwezekani Zungu kuweka Fedha hizo chafu Benki kwa kuwa anaogopa atagundulika na Mamlaka.

    Zungu maafa kwa uchache aliyoiletea nchi yake Mexico na dunia ni:

    1.Ukosefu wa ajira,
    2.Kudumaa kwa Uchumi,
    3.Kudorora kwa Biashara,
    4.Kama tunavyoona kwetu huku Afrika watu hata maji ya kunywa hawana sehemu zingine Mitaji hiyo ingekaa Benki labda Sekta Binafsi ingekopa na kuendesha Miradi ya huduma ya maji safi,
    5.Masoko kudorora.

    Hayo yote yakijiri duniani Bwana Guzman na mkewe wamelalia USD 22 Bilioni kwenye godoro lao chumbani!!!

    ReplyDelete
  7. Ehhh jamani Dola Bil. 22 zipo mkononi mwa mtu tu?

    Si mchezo ndio maana Uchumi wa 'Sembe' una nguvu sana duniani !

    ReplyDelete
  8. Kaazi kwelikweli!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...