Profesa Mark Mwandosya akila tizi mapema asubuhi hii mjini Dodoma. Ameiambia Globu ya Jamii kwamba yeye bila kukimbia asubuhi na jioni mwili humuwasha sana na hafanyi kazi vizuri. Kila siku anakimbia kilomita 2. Pia yeye ana mkanda wa kahawia wa Goju Ryu Karate, hivyo yuko fiti
Kamera yetu pia imewakamata Mhe. Cynthia Ngoye na Mhe.Amina Makilagi,Wajumbe wa Bunge maalumu la Katiba wakifanya mazoezi ya kutembea mapema leo mjini Dodoma. Mhe. Ngoye ametuambia kwamba wao hutembea umbali wa kilomita 3 kila siku katika kujiweka sawa kimwili na kifikra kabla ya kuingia bungeni. Chini ni Mhe Yahya Kassim Issa,ambaye ni bingwa wa Marathon Bungeni
Wajumbe Mhe.Zarina Madabida na Mhe.Zainab Vullu, wakitembea. wao wanasema hukimbia kilomita moja na kutembea kilomita mbili kila siku asubuhi. Mhe Vullu pia ni Centre mzuri sana kwenye Netball wakati mama Madabida anapenda kuwa refa tu
Upande wa pili wa mji wa Dodoma tumekutanma pia na wajumbe Mhe.Yahya Kassim Issa na Mhe.Prof.Makame Mbarawa wakifanya mazoezi.  Waheshimiwa hawa wanasema wao hutembea umbali wa kilomita 5 kila siku asubuhi ili kujiweka sawa na majukumu ya kila siku.
Hawa hawajasema wanapenda mchezo gani lakini kuna fununu wako fiti sana katika kuogelea
Mhe.Haji Fakih Shaah na Mhe Said Ali Mbarouk pia hawakosi katika kupasha moto viungo kila asubuhi na jioni. Hawajatuambia wao ni mabingwa wa mchezo gani ila Mhe Shaah anasifika kwa soka na Mhe Mbarouk kacheza sna hockey alipokuwa skuli
Mhe.Stephen Masele,Mjumbe pekee anayecheza mchezo wa kutupa tufe na mkuki. Naye hakosi kula tizi kila kukicha




Mjumbe Mhe.Mwanakhamis Kassim Said pia hakosi kujilawa kila asubuhi kukimbia na kutembea mjini Dodoma. Anasema yeye pia ni mcheza Judo na anasikitika hana patna wa kufanya naye mazoezi hapa Dodoma

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Mdau Lubida - SwedenMarch 13, 2014

    Thanks Ankal kwa picha hizi. ni muhimu kurekodi vitu hivi na ku broadcast hata kwenye TV ili kuhamasisha michezo katika jamii. Inafurahisha sana

    ReplyDelete
  2. Webgine wanazuga tu. Tizi peke yake siyo tija, tizi na lishe bora ndo tija.

    ReplyDelete
  3. Hongereni waheshimiwa mtu ni afya!

    ReplyDelete
  4. Mazoezi ni survivor kwa wote waliozidi miaka 40, kama ufanyi zoezi lolote na umefifikia au kupita umri huu hujitakii mema kiafya. Sana sana kutembea haraka haraka nusu saa kwa siku ni vizuri kwa afya (brisk walk)

    ReplyDelete
  5. Safi sana waheshimiwa!!

    Akikimbia Lowasa watu ooh, kalipa waandishi wampige picha.....sam pipo bwana, hooovvyooo!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...