Baadhi ya akina mama wanaojishughulisha na biashara ya samaki,wakiwa wametoka bandari ya Kabwe,Wilayani Nkasi mkoani Rukwa mapema leo,ambapo dishi moja kama uonavyo pichani huuzwa kati ya shilingi Elfu 30,000/=
Akina mama wakiwa na madishi yao ya samaki,akina mama wengi eneo hilo wameeleza kuwa wanafaidika na biashara hiyo ya samaki kwa kujiingizia kipato na hatimaye kujikwamua na ugumu wa maisha,wameeleza kuwa changamoto yao kubwa ni mitaji ya kutosha ili kuendeleza biashara hiyo ambayo Wanawake wengi hujishughulisha nayo.
Dishi lililobebwa samaki aina ya Migebuka huuzwa shili Elfu Thelathini
Wavuvi wakirejea baada shughuli yao ya uvuvi kufanyika katika bandari ya Kabwe,Wilayani Nkasi mkoani Rukwa mapema leo.
Picha na MichuziJr-MICHUZI MEDIA GROUP-NKASI RUKWA
Picha na MichuziJr-MICHUZI MEDIA GROUP-NKASI RUKWA
Wanawake hawa wamejitahidi kufanya biashara ya samaki. Kutovaa kwao viatu au hata ndala katika picha ya kwanza kunaonyesha biashara bado haijachanganya.
ReplyDeleteYaani dola mbili unapata dishi zima......hahahaha wakati hapa Sweden kwa hela hiyo hupati Samaki hata utoke chozi la damu.....Duh..ebwana weee dishi zima? au kuna makosa ya kiuandishi???
ReplyDeleteMdau wa kwanza.....ebu tafakari kauli yako kwanza,hao ni wafuasi wa Mrisho Mpoto, wanapata eneji toka ardhini na kuisambaza mwilini....hujamsikia Mpoto wewe au?
ReplyDeleteMdau wa pili naona hesabu ni ngumu kidogo kwako. Dola mbili ni Tshs. elfu thelathini??Jaribu hiyo hesabu tena tafadhali!
ReplyDelete