Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, Mhe Anthony Mataka(Kushoto) akiwa na wataalamu wa lishe toka USAID Tuboreshe chakula, akishiriki kwa vitendo  kuandaa uji wa mtoto wa miezi 6 hadi miaka 5 kwa kuchanganya virutubishi tayari kwa kumnywesha mtoto katika kampeni za uhamasishaji na uelimishaji wa virutubishi, katika viwanja vya Shule ya msingi Mafisa A mkoani Morogoro. Kampeni hizi zimedhaminiwa na shirika la misaada la marekani USAID Tuboreshe chakula.
Mkuu wa wilaya Mvomero, Mhe. Anthony Mataka akimnywesha uji, mmoja wapo wa watoto waliohudhuria sherehe za uzinduzi wa siku ya Virutubishi viwanja vya shule ya msingi Mafisa A,mkoani Morogoro. lengo la kampeni ni kuhamasisha,kuelimisha umuhimu na faida za virutubishi kwa watoto walio na umri kati ya miezi 6-miaka 5. Kampeni hizi zimefadhiliwa na Shirika La misaada la Watu wa Marekani (USAID) kupitia Mradi wa Tuboreshe Chakula.
Mkuu wa wilaya Mvomero, Mhe. Anthony Mataka (kushoto) akiteta jambo na Mshauri wa Rais mambo ya lishe,Dkt. Wilbrad  Lorri wakati wa sherehe za uhamasishaji wa virutubishi kwa watoto umri wa miezi 6-miaka 5 Mkoani Morogoro. Kampeni hii iko chini ya mradi wa Tuboreshe Chakula unaofadhiliwa na Shirika la Misaada la Watu wa Marekani USAID.
Mtaalamu wa lishe Nuria.K.Majaliwa akitoa mafunzo juu ya virutubishi na umuhimu wa unga lishe,kwa aliyekua mgeni rasmi Bw Anthony Mataka Mkuu wa Wilaya ya Mvomero. Pembeni yake ni Mkurugenzi Mkaazi wa USAID Tuboreshe Chakula, Bi. Rebecca Savoure katika sherehe za uzinduzi wa siku ya virutubishi.Lengo ikiwa ni kusisitiza na kuelimisha faida na umuhimu wa virutubishi kwa watoto umri wa miezi 6 – miaka 5, ikiwa ni mkakati wa Serikali ya Tanzania,ikishirikiana na USAID tuboreshe chakula kupunguza utapiamlo nchini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...