Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mh. Saidi Mecki Sadiki (kushoto) akizungumza na mkazi wa eneo la Mloganzila Bw. Fredy Justine Masondole (kulia) ambaye aliweka pingamizi kuzuia miundombinu ya maji, umeme na barabara kupita katika eneo lake , Hata hivyo mkazi huyo aliruhusu ujenzi kuendelea baada ya mazungumzo ya kupatikana kwa muafaka kufikiwa. Katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa TANESCO Mhandisi Felchian Mramba.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mh. Saidi Mecki Sadiki (katikati) akizungumza jambo wakati alipotembelea eneo la ujenzi wa Hospitali na Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi cha Muhimbili(MUHAS) lililo kwenye mpaka wa wilaya ya Kisarawe na mkoa wa Pwani leo.Wengine kutoka kushoto ni Katibu Tawala wa mkoa wa Dar es salaam Bi.Therezia Mmbando,Mkurugenzi Mkuu wa DAWASA Bw. Archard Mutalemwa na Meneja wa Tanroad mkoa wa Dar es salaam Bw. Ndyamukana Julius.
Mkazi wa eneo la Mloganzila Bw. Fredy Justine Masondole (Katikati) akiwapeleka katika eneo la nyumba yake lenye mgogoro viongozi wa mkoa wa Dar es salaam wakiongozwa na Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Saidi Mceki Sadiki (upande wa nyuma katikati), mkuu wa wilaya ya Kinondoni Jordan Lugimbana na Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es salaam Bi. Theresia Mmbando.
Mafudi wakiendelea na ujenzi wa awali wa ofisi za muda katika eneo itakapojengwa Hospitali na Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi cha Muhimbili(MUHAS) lililo kwenye mpaka wa wilaya ya Kisarawe na mkoa wa Pwani leo Picha na Aron Msigwa - MAELEZO.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. MKAZI HUYU ANAZO HAKI ZAKE NA NILAZIMA ZIHESHIMIWE HATA KAMA HANA JINA KUBWA, VIONGOZI WASIPENDE KUTOA AMRI ZA VITISHO KATIKA KUTATUA JAMBO AMBALO LINGEWEZA KUMALIZWA KIRAHISI BILA KWENDA MAHAKAMANI.

    ReplyDelete
  2. Haya maeneo yanahitaji maendeleo, tusikwamishe au kuchelewesha ujenzi wa hospitali kubwa.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...