WATAALAMU MBALIMBALI NCHINI WALIOSOMA USSR WALIFANYA SHEREHE KUBWA SIKU YA JUMAMOSI TAREHE 08.08.2014 KWENYE HOTEL YA ANGITTHI ILIYOPO KWENYE BARABARA YA ALLY HASSAN MWINYI MAENEO YA VICTORIA JIJINI DAR-ES-SALAAM.

KATIKA SHEREHE HIYO ILIYOANZA SAA 12.30 JIONI HADI SAA 5.45 USIKU, WASOMI HAO WAKIONESHA IMANI KUBWA KWA DTR. AZIZI MRIMA KWA KUMPONGEZA NA KUMPA ZAWADI KWA KUTEULIWA KWAKE KUWA BALOZI WA TANZANIA NNCHINI MALAYSIA NA KUAHIDI KUMPA USHIRIKIANO WA KARIBU KATIKA KAZI ZAKE ZA KILA SIKU, NA KWA WAKATI TOFAUTI WASOMI HAO WALIMUOMBA MH. BALOZI KUFUNGUA FURSA NYINGI KWA WAWEKEZA NA HASA KUKUZA WIGO WA USHIRIANO WA KIBIASHARA BAINA YAO NA WATAALAMU WA KIMALAYSIA.

WASOMI NAO WALIOMBWA KUJIAMINI NA KUJITUMA KWANI ELIMU WALIYOPATA USSR NI DHAHABU NA HAZINA KUBWA NA KWAMBA WATAALAMU WENGI NCHINI NA BAADHI YA VIONGOZI WAKUBWA HIVI SASA WALIOSOMEA USSR. AITHA KATIKA SHEREHE HIYO WATAALAMU HAO WALIMPONGEA BW. FELIX NGAMULAGOSI KWA KUTEULIWA KWAKE KUWA MKURUGENZI MKUU WA EWURA.
Mh. balozi Dkt. Azizi Mrima akikabidhiwa zawadi aliyoandaliwa na waliosoma USSR. Anayekabidhi zawadi hiyo ni mjumbe wa kamati ya maandalizi ya sherehe ambaye pia ni Mkurugenzi wa utawala wizara ya Ulinzi Alhaj Zakaria Kera "Bob Zii" , Anayepiga makofi kushoto kushoto kwa mh. balozi ni mwenyekiti wa kamati Dkt. Suphian Masasi na kulia kwa Mh. balozi ni Mjumbe wa kamati na daktari bingwa wa mifupa MOI Dkt. Paul Mareale.
Baadhi ya wataalamu waliosoma USSR wakipata mlo rasmi wa pamoja kwa heshima ya Mh. Dkt. Azizi Mrima katika moja ya matukio kwenye sherehe ya kumpongeza kuteuliwa kwake kuwa balozi wa Tanzania nchini Malaysia.
picha ya pamoja ya baadhi ya waliosoma USSR wakipozi pamoja na Mh. balozi dkt. Azizi Mrima katika moja ya matukio ya kumpongeza. Katikati waliokaa mwenye shati la mkono mirefu ndiye mpongezwa Mh. Balozi wa Tanzania nnchini Malaysia Dkt. Azizi mrima,mwisho kushoto mwenye koti na suruali nyeupe ni Ing. Dkt. Suphian Masasi (mwenyekiti wa kamati ya maandalizi), mwenye suti na tai ni mh. Felix ngamulagosi (Mkurugenzi Mkuu EWURA), akifaatiwa na Dkt.Koti Kamanga (kulia kwa balozi) baada ya mh. balozi Dkt. Lucy Mareale, Mrs Katete, Mrs. Kera akifuatiwa na Dkt. Paul Mareale na mwisho (mwenye shati jekundu) ni Mkurugenzi wa tiba na Ufundi wa Bima ya afya ya wananchi Dkt. Likei .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...