NMB imezindua rasmi tawi la jipya la Buzuruga mkoani
Mwanza, likiwa ni tawi la tisa kuzinduliwa katika mkoa wa huo, huku
NMB ikiendelea kuwa ndio benki yenye matawi mengi zaidi Tanzania.
Akizungumza katika sherehe ya ufunguzi huo, Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana,
Mh. Baraka Konisaga ameipongeza benki ya NMB kwa hatua nyingine
iliyopiga kwa kusogeza zaidi huduma kwa
wateja na kuitaka iendelee kuwa kinara
wa huduma za kibenki nchini.
Aliwahamasisha wafanyabiashara, wakulima na
wafanyakazi waitumie fursa ya kuwepo kwa tawi la NMB Buzuruga kukidhi mahitaji
yao ya kibenki. Vilevile, aliwasihi wananchi waache kuweka fedha kwenye chaga
za vitanda na badala yake watumie njia salama ya kuweka fedha benki.
“Ni matumaini
yangu kuwa uwepo wa tawi hili la Buzuruga ni neema kubwa kwa wakazi wa
Mabatini, Buzuruga, Nyakato, Igoma, Kishili, Buswelu na hadi Kisesa hasa
wafanyabiashara katika hizi mashine za mpunga kwani kesi za watu kuporwa fedha majumbani
au maofisini zitapungua badala yake ongezeko la wateja wanaofungua akaunti ndio
itakua habari ya eneo hili” alisema Konisaga.
Kwa upande wake, Bw. Straton Chilongola, ambae
ni Meneja wa NMB Kanda ya Ziwa, alisema “Tangu
kuanzishwa kwa tawi hili tumeshuhudia wakazi wengi wa wakija kufungua akaunti na
kutumia huduma za benki hii. Hii ni uthibitisho kuwa wakazi hawa walikua na kiu
ya kupata huduma za kibenki karibu kariba na milangoni kwao. Lakini pia tutaendelea kubuni mbinu mbalimbali zitakozotuwezesha
kuwafikia wateja wetu karibu zaidi ili kuondoa msongamano kwenye matawi na pia
kuokoa muda wa wateja ili waweze kutumia muda wao kwa shughuli endelevu.”
Tawi hili la Buzuruga, linatoa huduma zote za
kibenki, ikiwa ni pamoja na huduma ya mikopo ya aina mbali mbali bila kusahau
mikopo ya Kilimo. Tawi hili litakua wazi kila Jumatatu
hadi Ijumaa kuanzia saa mbili na nusu asubuhi hadi saa kumi na jioni ( 2:30
asubuhi - 10:00 jioni) na Jumamosi
kuanzia saa mbili na nusu asubuhi hadi saa sita na nusu mchana (2:30 asubuhi -
6:30 mchana), Jumapili na siku za Sikukuu hakutakuwa na huduma ndani ya tawi
hili. NMB daima benki
yako!
Kikundi cha ngoma cha Bujora kikitumbuiza katika hafla ya
uzinduzi huo.
Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya wa Nyamagana, Bw. Baraka Konisaga akikata utepe
kuashiria uzinduzi rasmi wa tawi la NMB Buzuruga. wakishuhidia uzinduzi huo kutoka kushoto ni Naibu Meya Jiji
Mwanza mhe. John Minja, Mkurugenzi wa jiji
la Mwanza Bw. Halifa H. Hida na kutoka
kulia ni Meneja wa NMB Kanda ya Ziwa, Bw. Straton Chilongola, Meneja Tawi la
NMB Buzuruga, Gadiel Sawe na Meneja Mawasiliano wa NMB , Josephine
Kulwa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...