Na Kibada Kibada –Katavi
Wananchi wa Halmashauri ya wilaya ya Mpanda wamepewa changamoto kutunza vyanzo vya maji na kuhifadhi mazingira kwani kuharibu mazingira kunapelekea kuchangia ukame na kukosekana na maji ambayo ndiyo uhai wa viumbe na tegemeo la maisha ya wanadamu na wanyama.
Changamoto hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mpanda Kibiriti Yasini wakati akiwahutubia wakazi wa kijiji cha Milala Kata ya Kabungu kwenye maandalizi ya wiki ya maji inayotarajiwa kufanyika kilelele cha machi 22 mwaka huu.
,Kibiriti mewataka kutoa ushirikiano wa karibu kila mtu kwa nafsi yake kuhakikisha anatimiza wajibu wake katika kulinda,kutunza na kuhifadhi mazingira kwa faida ya vizazi vilivyopo na vijavyo.
Katika hotuba yake hiyo alisisitiza wananchi watoe ushirikianao wa thati kutunza vyanzo vya maji na kuilinda miradi ya maji iliyopo katika katika kijiji hicho na kuiona kuwa ni mali yao na itawasaidia kwa manufaa ya wote hivyo ni wajibu wao kuitunza na kulinda. Kwa kuwa mradi wa ,maji uliopo hapo kijijini utawaondolea kero ya muda mrefu iliyokuwa ikiwabaili hasa wanawake na watoto ndio wanaotabika kwa kukosa maji sehemu yeyote ile.
Akizungumzia maandalizi ya wiki ya maji kila mwaka alisema kila mwaka huambatana na utoaji wa elimu juu ya utunzaji wa mazingira,na uhifadhi wa vyanzo vya maji ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa ilani ya chama tawala,kwa kutambua umuhimu serikali imefanya juhudi za kuhakikisha inwaondolea wananchi wake kero ya upatikana wa maji na kuwasogezea karibu wananchi maji.
Alieleza kuwa Katika kijiji cha milala vituo kumi vya kuchotea maji vimejengwa na wananchi watapata maji hivyo kuwaondolea kero iliyokuwa ikiwakabili wakazi hao na Halmashauri yake kwa kushirikiana na Serikali kuu kwa kutekeleza mpango wa matokeo makubwa sasa Big Results Now (BRN).
Hata hivyo amemwagiza Kaimu Mhandisi wa maji katika Halmashauri hiyo kuhakikisha wananchi wa kijiji cha Milala kero ya ukosekanaji wa maji inakwisha kwa kuwa halmashauri imejipanga kutekeleza na kuwaondolea kero hizo.
Kwa upande wa upatikanaji wa maji katika halimashauri ya wilaya ya Mpanda ni wastani wa asilimia 48 tu ambapo hali hiyo ni kiasi kidogo lengo ni kuhakikisha asilimia hiyo inaongezeka angalau kila kijiji kiwe na maji ya uhakika.
Aidha aliwaeleza wananchi hao kuwa ifikapo juni 2014 miradi ya maji ya katika vijiji vya Isenga Kata ya MIshamo,Ikola Kabungu na Karema itakuwa imekamilika kwa karibu asilimia 75,na kwasisistiza kuwa miradi hiyo ni mali yao waitunze na kuienzi pia wanachangia mifuko ya maji ili kuimarisha mifuko kwa kuwa na mifuko wa maji utasaidia katika matatizo madogo madogo yanayojitokeza katika maradi kama ukarabti kwa kununua vifaa vidogovidogo vya matengenezo ili maji yaendelee kuwanufaisha wananchi.
Awali Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Milala Rosemary Omera akisoma taarifa ya kijiji alieleza kuwa kijiji kilikuwa kinakabiliwa na matatizo ya maji lakini kupatikana kwa mradi wa maji katika kijiji hicho kumesaidia kwaondolea kero iliyokuwa ikiwakabili.
Ingawa wakazi wa kijiji hicho wanakabiliwa na changamoto ya uharibifu wa mazingira unaoambatana na uingiaji wa mifugo kiholela hali inayochangia uharibifu wa mazingira na hasa vyanzo vya maji katika maeneo mengi hapa kijijini.
Akawataka wananchi wajenge utamaduni wa kutunza na kuhifadhi mazingira ili kusaidia kuhifadhi vyanzo vya maji pia aliomba serikali iendelee kuwaletea miradi mingine ya maji na has katika shule ya Sekondari y ufundi ya Milala amabayo inakabiliwa na tatizo la maji safi na salama.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda Yasini Kibiriti akiwahutubia wananchi wa kijiji cha Milala Kata ya Kabungu Wilayani Mpanda wakati wa maandalizi ya maazimisho ya wiki ya Maji sherehe zilizofanyika kwenye uwanja wa mikutano Kijiji cha Milala.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Milala waliofika kujumuika na wazazi wao katika sherehe za maandalizi ya wiki ya Maji, kama ilivyo kwa wanafunzi kujenga tabia ya kusoma alikuwa alikuwa akisoma gazeti la Mpandaleo linalotolewa na Halmashauri ya wilaya ya Mpanda, mwanafunzi huyo alikuwa akisubiri mchakato wa mzima wa sherehe za maandalizi akiwa na wananfunzi wenzake waliofika kushuhudia maandalizi hayo .
Wakazi wa kijiji cha milala wakichuana kunywa pombe ya kienyeji aina ya Komoni katika kusherehesha maandalizi ya wiki ya maji katika halmashauri ya Mpanda mshindi katika mpambano huo alijinyakulia kitita cha shilingi elfu kumi.
Ejamani weee!
ReplyDeleteHaya mashindano ya Kunywa Pombe Pana watu wa Huduma ya Kwanza na vifaa cyao karibu?
Yasije yakatokea yale yale ya Kigogo Mbuyuni kwenye mauaji ya watu 11 mwaka 2011 baada ya 'Mtindi' kuvuka viwango vya TBS ktk unywaji wa Gongo !!!
jamani nchi ziliziendelea mnadai wanachanganyikiwa na ushoga.nchi zetu nazo naona zinaanza kuchanganyikiwa kivyake.Naona kundi kubwa la wanafunzi kunywa pombe ni message gani mnawapa hao watoto? waandaaji inabidi waiombe radhi jamii.Michuuuuuzi kulikoni hadi naona hasira.
ReplyDeleteHivi hayo mashindano yanatoa somo gani kwa hao wanafunzi? Mambo mengine hayahitaji kufikiria sana kuona kwamba ni mabaya. Shame on you
ReplyDeleteBadala ya watu kunywa maji wanashindana kunywa pombe....only in Bongoland kwenye kusheherekea wiki ya maji.
ReplyDeleteNa wanafunzi ndani ya uniform wanashangilia kwa nyuma, ujinga mtupu huu
ReplyDeleteHII SI PICHA NZURI KWA JAMII HASAA WATOTO
ReplyDeletePombe na uzinduzi wa maji wapi na wapi ??
ReplyDeleteEbu tuwe na fikra endelevu!
si walau wangefanya mashindano ya kunywa hayo maji?
WEWEEE CHEZEA TANZANIA WEWE?HAYA NDIO MAMBO YANAYOTUPA SIFA KIMATAIFA BWANA......POMBE,KUKANYAGISHWA NA WAGENI,KUPIGWA CHANGA.....KULIALIA SHIDA NA MENGINEYO........
ReplyDeleteMdau wa 7 hapo ju:
ReplyDelete''Pombe na Maji wapi na wapi?''
Uhusiano upo mwanawane,
Ndugu yangu hujasikia watu wakisema 'AMECHAPA MAJI HADI AKAANGUKA CHINI''?
Pombe za Kienyeji:
ReplyDeleteAngalieni wazee hao watatu wanatamani Mpango huu uwepo kila wiki ili waweze kuchaguliwa na kuchapa masanga ya bure ya Udhamini.
Kwa wakazi wa vijijini ndio tumaini lao la mwisho la kujiliwaza baada ya kazi ngumu za mashambani!!!
Ndugu zetu Majuu mneona Gilbeys, Vodka na Buddweiser zetu za Kienyeji?
ReplyDeleteHao jamaa wanywaji ukiwapa za maji ya huko kwenu ng'o hawalewi !
Jamaa wa 3 wanashukuru sana kwa kuchaguliwa kuwakilisha!
ReplyDeleteSi mnajua Ukata wa vijijini Elfu moja ya kupata walau Kopo moja la maji ni kama LAKI MOJA?
hahaha...Nimechekaje sasa, kazi kweli kweli hii nchi, jamani Elimu inatakiwa sana, sasa hapa wanasherekea siku ya maji au wanatangaza pombe aina ya kommon,
ReplyDeletehuo ndio urithi wetu jamani.
ReplyDelete