Wanawake wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wameungana na Wanawake wengine kote duniani katika kusheherekea Siku ya Wanawake Duniani, iliyofanyika katika Viwanja vya Mwembe Yanga Temeke, jijini Dar es Salaam. Mgeni rasmi kwenye maadhimisho hayo alikuwa ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Hawa Ghasia (Mb.). Kauli mbiu ya maadhimisho ya mwaka huu ni "CHOCHEA MABADILIKO KULETA USAWA WA KIJINSIA"
Wanawake wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wakiwa katika maandamano.
 Mhe. Ghasia (wa tatu kutoka kushoto) akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Said Mecky Sadick pamoja na wageni waalikwa katika jukwaa wakiwashangilia Wanawake wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa (hawapo pichani) walipokuwa wakipita mbele yao .
Wanawake wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wakipita mbele ya mgeni rasmi (hayupo pichani) wakiwa wamejawa na furaha.
Wanawake  kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wakiwa katika Picha ya Pamoja. 
Picha na Reginald Kisaka

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Hongereni wanawake wote na mlionekana kwenye picha mmependeza kweli kweli.

    ReplyDelete

  2. Nawaunga mkono ila mabadiliko muyafanye ninyi kwa kufanya jitihada tangu shuleni kule msingi. mtoto wa kike anakaa nyuma darasani, aogopa, n.k.afikiria kuolewa ili atunzwe na wachapakazi.

    Mi binti yangu namfunza kila kitu awezacho mwanamme, kubaili tairi, kufanya hesabu, kufikiri na kutowa mawazo mazuri zaidi ya wanaume, nk.

    Tatizo ni kutaka kufanikiwa kwa kuwezeshwa (ikimaanisha mafanikio yenu lazima mwanaume abanwe). Mfano, kazi hii asipewe Joseph apewe Josephina ili pawepo mwanamke pia, bila kujali ubora. La, inatakiwa kujenga uwezo wa kumiliki soko la ajira. Dunia hii ni kusavaivu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...