Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Mabibo Beer ambao ni wauzaji wa vinywaji vya Windhoek na Climax, Mama Benadetha Rugemalila akikabidhi baadhi ya misaada kwa Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mwananyamala, Bw Kariamel Wandi wakati Kampuni ya Mabibo Beer wakishirikiana na Wasanii wa Bongo movie walipotembelea Hospitali ya Mwanyamala ikiwa wanaadhimisha miaka mitatu ya Kuanzishwa kwa Klabu ya Bongo Movie.
Wasanii wa Bongo Movie wakiwa katika picha ya pamoja na mkurugenzi mkuu wa Mabibo beer na Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mwananyamala mara baada ya wasanii wa bongo movie na Kampuni ya Bia ya Mabibo kutembelea na kukabidhi misaada katika hospitali ya Mwananyamala mapema leo.
 Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Mabibo Beer, Mama Benadetha Rugemalila(kulia) akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kukabidhi misaada katika Hospitali ya Mwananyamala leo, Katikati ni Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mwananyamala, Bw Kariamel Wandi na Mwenyekiti wa Klabu ya Bongo Movie Tanzania.
 Kaimu Mganga Mkuu wa hospitali ya Mwananyamala, Bw Kariamel Wandi (kulia) akitoa maelekezo kwa Wasanii wa bongo movie pamoja na Mkurugenzi mkuu wa Kampuni ya Mabibo Beer, Mama Benadetha Rugemalila (pili kulia) ambao ndio wauzaji na wasambazaji wa Vinywaji vya Windhoek na Climax wakati walipotembelea Hospitali ya Mwananyamala leo kwaajili ya kutoa Misaada mbalimbali kwa wagonjwa ikiwa ni maadhimisho ya miaka 3 ya Kuzaliwa kwa Klabu ya Bongo Movies huku Kampuni ya Mabibo Beer ikiwa wadhamini wakuu wa Bongo Movie.
 Wasanii wa bongo movie wakielekea kwenye wodi za wagonjwa katika hospitali ya mwananyamala mapema leo kwaajili ya kutoa misaada kwa wagonjwa wakati bongo movie wakiadhimisha kilele cha Miaka 3 tokea kuanzishwa kwake.
 Bi Sada Abasi (kushoto) akipokea misaada kutoka kwa mmoja wa wasanii wa bongo movie ambao walitembelea hospitali ya Mwanyamala leo ikiwa wanaadhimisha miaka 3 ya kuzaliwa kwa Klabu ya Bongo Movie.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...