DSC_1151
Meneja Huduma Maji taka kutoka Dawasco, Mathias Mulagwande (mwenye suti ya damu ya mzee) akinyoosha kidole kumuonyesha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadick (wa pili kulia) sehemu korofi za kutiririsha maji machafu barabara ya Morogoro kati kati ya jiji. 

Na Damas Makangale

WATENDAJI wa Mamlaka za Maji Safi na Taka, Manispaa, Halmashauri, Wakala wa Barabara na Mabasi yaendayo kasi wameshauri kuwa na utaratibu wa kuwasiliana na kushirikiana kwa pamoja ili kuleta tija katika usombaji taka katika jiji la Dar es Salaam.

Akizungumza na mwandishi wetu, kwenye ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mh Said Meck Sadick, Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Green Waste Pro Ltd. Bw. Anthony Mark Shayo amesema kuwa tatizo la jiji la Dar es Salaam ni watendaji wa mkoa hawana mawasiliano ya kutosha katika utendaji kazi wa kila siku.

Shayo alizungumza hayo kwenye ziara hiyo ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ya kugagua hali ya usafi katika maeneo kadhaa pamoja na kuangalia maeneo korofi katika kutitirisha maji machafu kwenye mitaro kadhaa kati kati ya jiji.

“tatizo kubwa katika jiji la Dar es Salaam ni watendaji wa jiji, manispaa, wakala wa barabara, Tanesco na mamlaka za maji safi na taka kutokuwa na  utaratibu wa kuwasiliana katika utendaji kazi wa kila siku katika kuboresha usombaji wa taka kwenye jiji la Dar,” amesema Shayo
DSC_1173
Meneja Huduma Maji taka kutoka Dawasco, Mathias Mulagwande akiwaonyesha baadhi ya viongozi wa Mkoa wa Dar es Salaam, akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Dar, Said Meck Sadick na Mbunge wa Ilala, Mussa Zungu baadhi ya mashimo (Potholes) ambayo ni hatari kwa wananchi watembea kwa miguu baada ya ujenzi wa barabara ya mabasi yaendayo kasi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Ushauri wangu kwa jiji la Dar es Salaam, naomba wafungwa watumike katika kufanya usafi wa jiji hasa kwa wale wanaokaribia kumaliza kifungo ambapo itakuwa ngumu kutoroka. Wafungwa wanakaa bure ndio maana wanafanya uwalifu wa makusudi wakijua jela kula na kulala.

    wafanye kazi za ujenzi kuliko kujaza kila mahali wachina.

    ReplyDelete
  2. Kidhungu jamani shida
    Kuna mtu na wifi yake,aliyopo kwenye picha ni manhole siyo pothole.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...