Waziri Mkuu Mizengo Pinda (kushoto) akimkabidhi mfano wa hundi ya shilingi milioni tano Dk. Maria Kamm aliyetwaa Tuzo ya Mwanamke Bora wa Mwaka 2013/2014 ndani ya Ukumbi wa African Dreams uliopo Area D, Dodoma jana usiku.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda (kushoto) akimvisha medali ya Mwanamke Bora wa Mwaka 2013/2014, Dk. Maria Kamm.
Waziri Mkuu akimkabidhi tuzo, Anna Margareth Abdallah, kwa niaba ya mshindi wa pili ambaye ni Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Asha-Rose Migiro.
Waziri Mkuu akimkabidhi tuzo Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi Profesa Anna Tibaijuka aliyeibuka mshindi wa tatu katika tuzo hizo.
Mbunge wa Same Mashariki (CCM), Anne Kilango Malecela, akipokea tuzo kutoka kwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda baada ya kushika nafasi ya nne.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda (katikati) katika picha ya pamoja na washindi walioingia Nne Bora. Kutoka kushoto; Anna Abdallah aliyechukuwa tuzo kwa niaba ya Dk. Asha-Rose Migiro, Anne Kilango Malecela, Dk. Maria Kamm na Profesa Anna Tibaijuka.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Hongera saana kina mama wote
    Mchango wenu kwa Taifa ni mfano
    mzuri wa kuigwa na kizazi kipya.
    Mikidadi-Denmark

    ReplyDelete
  2. Neno shujaa lina tafsiri nyingi sana......

    ReplyDelete
  3. hapana, neno shujaa lina maana moja tu ila watu wameanza kulitumia pasipo penyewe.

    ReplyDelete
  4. Hongera kina mama muendelee kuhamasisha wakina mama wachangamke siyo kukaa tu bila mpango wowote wakutoa mchango katika jamii.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...