Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akimpokea Binti Mfalme wa Sweden, Mtukufu Victoria Lugrid Alice Desiree mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Kambarage Nyerere, nchini Tanzania kwa ziara ya kikazi ya siku tatu kuanzia Tarehe 19 hadi 21 Machi, 2014.
Mhe. Membe akiwa katika mazungumzo na Binti Mfalme wa Sweden, Mtukufu Victoria Lugrid Alice Desiree mara baada ya kuwasili nchini.
Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Dora Msechu kwa pamoja na wajumbe walioambatana na Binti Mfalme Victoria Ludrid Alice Desiree nchini wakifuatilia kwa karibu mazungumzo kati ya Mhe. Membe na Binti Mfalme wa Sweden, Mtukufu Victoria (hawapo Pichani).
Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bi. Victoria Mwakasege pamoja na Afisa Mambo ya Nje Bi. Tunsume Mwangolombe wakati wa mazungumzo kati ya Waziri Membe na Binti Mfalme Victoria Ludrid Alice Desiree (hawapo pichani).Picha na Reginald Philip.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...