Timu ya Yanga SC imeondolewa kwenye Michuano ya Klabu Bingwa Barani Afrika baada ya kufungwa na Al Ahly kwa penalti 4-3 katika mechi iliyochezwa usiku huu Uwanja wa El Max Haras El Hodod jijini Alexandria, Misri.

Mpaka dakika ya 90 ya mchezo, matokeo ya jumla yalikuwa 1-1 (mchezo uliisha kwa Al Ahly kuifunga Yanga bao 1-0 kama walivyofungwa wao Dar es salaam) Hivyo kuamriwa kupigwa mikwaju ya penalti ambapo Yanga walipata mabao 3, wakati Al Ahly walipata mabao 4.
Wachezaji wa Yanga waliofunga penalti ni Didier Kavumbagu, Emmanuel Okwi na Nadir Haroub 'Cannavaro' wakati Oscar Joshua, Mbuyu Twite na Said Bahanuzi walikosa mikwaju hiyo.
Kwa matokeo hayo, timu ya Al Ahly imefuzu katika hatua ya 16 bora ya michuano hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Hakuna cha kutolewa kiume hapo. Wametolewa just that simple, nendeni sasa mkakune nazi. Kila mwaka ndio matokeo hayo hayo

    ReplyDelete
  2. Pilau la Maulidi ya Ugenini mara zote halikosi kizungu mkuti!!!

    Utaona moja wapo la haya linatokea:

    1.Mchuzi wa kachumbari kuwa na pilipili nyingi sana.

    2.Ubwabwa kuwa wa moto sana, kwa kutolewa jikoni na kugawiwa papo kwa papo.

    3.Walaji kuwa wengi na masinia machache hivyo wengine kuambulia kapa baada ya ubwabwa kwisha wakisubiri masinia.

    Poleni wana Yanga S.C !!!

    ReplyDelete
  3. Yanga wamepoteza muda mwingi kuongea sana baada ya kushinda mechi ya kwanza wakaacha kufanya maandalizi ya maana na haya ndio matokeo yake. Warudi nyumbani kumtafuta mchawi na kuanza kuvurugana kama kawaida ya timu zetu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...