·       Yatangaza facebook, whatsapp and twitter BURE
·       Sasa wateja kupata whatsapp, Facebook na Twitter bure kupitia yatosha bando
  kampuni ya simu za mkononi ya Airtel inayoongoza kwa kutoa huduma bora imezindua huduma ya kibunifu itakayowawezesha wateja wake kupata na kuunganishwa kwenye mitandao ya kijamii ya Facebook, Whatsapp na twitter BURE kupitia huduma ya Airtel yatosha.

Akiongelea kuhusu huduma hiyo Mkuu wa kitengo cha mawasiliano wa Airtel Bi Beatrice Singano Mallya alisema” sasa ni bure kabisa kwa wateja wetu wote wa Airtel kuunganishwa na mitandao ya kijamii ya Whatsapp, Facebook na Twitter. Airtel tunayofuraha kutoa nafasi kwa wateja wetu kuwasiliana na marafiki na familia kupitia mitandao hii ya kijamii bure bila makato yoyote, huku tukiendelea kuthibitisha kuwa Airtel Yatosha ni BABA LAO!”
Aliongeza kwa kusema mteja yoyote atakayenunua kifurushi cha data cha yatosha kuanzia sasa iwe ni cha siku, Wiki au Mwezi vifurushi vyao vya internet vya MB au GB  hazitakatwa katika matumizi ya Facebook, Whatsapp na Twitter na badala yake wataweza kutumia vifurushi vyao vya data kwenye kuperuzi katika mitandao mingine kama vile YouTube na mingine mingi kadri ya mahitaji yao”
Akiongea kuhusu namna ya kujiunga Meneja Masoko wa Airtel Bi Upendo Nkini alisema” ili kupata Whatsapp, Facebook na Twitter BURE wateja watatakiwa kupiga *149*99# kisha kuchagua kifurushi kinachowafaa na kuanza kufurahia BURE Whatsapp, Facebook na Twitter”
“Sambamba na hilo katika kuendeleza ubunifu na kurahisiaha upatikanaji wa vifurushi vya Yatosha,  tumewawezesha wateja wetu  kutumia simu za kununua vifurushi vya yatosha kwa ajili ya marafiki zao familia na kubaki wakiwa wameunganishwa na kufurahia mitandao hii ya kijamii ya Whatsapp, Facebook na  Twitter BURE, furahia kuunganishwa katika mawasiliano kupitia mtandao wa Airtel” aliongeza Nkini

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...