Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM, Taifa, Sadifa Juma (wapili kushoto) akiwasili kwenye Uwanja wa Mkutano eneo la Tanganyika Packers, Kawe Dar es Salaam, Jumapili, Aprili 27, 2014 ambako mbali na kuhutubia mkutano wa hadhara, alikabidhi vifaa vya michezo kwa timu mbalimbali za soka katika kata ya Kawe. Kulia ni Mwenyekiti wa UVCCM Kata ya Kawe, Lilian Rwebangila na Katibu wa UVCCM wa kata hiyo, Aisha Katundu na kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Kata hiyo Said Herry.
 Vijana wa CCM na wananchi kwa jumla wakimsindikiza Sadifa, kwa hamasa kuingia uwanjani
 Naibu Katibu Mkuu wa UVCCM (Bara) Mfaume Ali Kizigo akihutubia kwenye mkutano wa hadhara wa UVCCM uliofanyika viwanja vya Tanganyika Packers, Kawe Dar es Salaam, Jumapili ya Aprili 27, 2014, kumkaribisha Sadifa kuhutubia.
 Mwenyekiti wa UVCCM Kata ya Kawe Lilian Rwebangila akimkaribisha Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Sadifa Hamis Juma, kuhutubia mkutano huo wa hadhara kwenye Viwanja vya Tanganyika Packers, Kawe.
 Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Sadifa Hamis Juma, akihutubia mkutano wa hadhara huku shamrashamra zikitawala, kwenye Viwanja vya Tanganyika Packers, Kawe, Dar es Salaam, Jumapili Aprili 27, 2014.
 Sadifa (kushoto) akishuhudia wakati Katibu wa CCM wilaya ya Kinondoni, Athuman Shemsha, akimtawaza Kada wa CCM, Vincet Massawe, wakati wa mkutano wa hadhara wa UVCCM  uliofanyika Viwanja vya Tanganyika Packers, Kawe, Dar es Salaam, Jumapili, Aprili 27, 2014

PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. MBONA PICHA ZAIDI KUHUSU TUKIO HILI HAZIONEKANI?????

    ReplyDelete
  2. Majina mazuri kweli 'Tanganyika packers*Tanganyika board of medicine*...........

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...