Ankal akiwa na Mkuu wa Idhaa ya Kiswahili ya BBC Bw. Ali Saleh alipovamia kituo hicho kuwataka hali wadau. Ankal alifarijika na kufurahi mno kukuta kumbe bosi huyu ni Bwawa la Maini damu kama yeye. Ila alimkuta hana furaha sana kwa kuwa vijana wa Liverpool wameharibu plani ya kocha Brendan ya kubaki katika nne bora tu mwaka huu ili kucheza Europe Cup na sio kuchukua ubingwa mwaka huu. Maana inavyoelekea kombe linaenda Anfield, ambapo Ali Saleh anasema ah! tukishinda hatutolikataa ila sie tumepanga tulibebe mwakani na sio mwaka huu....!
Charles Hilary Mkwanda akicheza na Ze Fulanazzzzzzz
Ankal na Bi Zuhura Yunus. Kumbe bado katoto kadogoooo.....dah!
![]() |
Ankal na Salim Kikeke a.k.a 'Yul Bryner. |
Ankal akila selfie na wadau Mariam Omar na Peter Musembi.
Ankal akiwa na Alex Muriethi (aliyeketi) na 'shemeji' yetu Siraj Kalyango ambaye chupuchupu amuoe nanihii, ila alichelewa kuleta mahari, na mke kusombwa na maji mengine...
Ankal akila konozzzzz na Zawadi Machibya. Anatoa shukurani sana kwa BBC idhaa ya Kiswahili kwa ukarimu na ucheshi wao na kumpokea kwa moyo mkunjufu japo alifika hapo bila taarifa wala mihadi. Pia hapo BBC idhaa ya Kiswahili wana utamaduni wa kumkaribisha mdau yeyote kutoka Afrika kwa moyo mkunjufu na hata kumfanyia mahojiano kama inawezekana.
Mkuu Ankal ! Chonde chonde ! Baba Fulanazzzzz ! ya blog ya jamii lazima urudi nayo bongo tusije tukasikia oh! mara kuna jamaa kafika bei,Oh ! mara umeiacha makumbusho London ,tutakaye mkuta nayo mtaani tutampa za ki-kariakoo
ReplyDeletewadau
FFU Ughaibuni aka "Watoto wa Mbwa"
ankal naomba unitumie na mimi ze fulanas....
ReplyDeletehiyp imekaa poa. nice pics
ReplyDeleteAnkal,
ReplyDeleteUandishi wako wa utani ninaupenda sana na unanifanya nipate furaha siku nzima na mara zote ninachokisoma hapa hujua kuwa ni maneno ya Ankal, lakini unapopest kitu najua kuwa maneno hayo hayakuwa yako na hukuya hariri wewe.
Unakipaji cha hali ya juu cha uandishi Ankal. Ahsante kwa Tanzania kuwa na mtu kama wewe. Mtu asifiwe akiwa mzima na azione mwenyewe sifa zake apewazo na watu.
- Mr Mhoja - Sweden.
nilikua na hamu nimuone aysha yahya.huyo alex muriethi kiswahili chake kinachekesha sana wallah.yeye kwake "th" ni "dh"
ReplyDeleteTafadhali Uncle naomba umsalimie sana KIKEKE Salym!
ReplyDelete