Ankal akiwa na muasisi na mwanzilishi wa Fashion show nchini Tanzania Da' Farida Matata a.k.a Farida Fashion ambaye alianzisha mambo ya fashion show miaka ya 1986 na kuwatoa warembo wengi kitaifa na kimataifa. Hivi sasa anaendesha biashara kibao jijini London ikiwa ni pamoja na mkahawa wa vyakula vya Kiswahili sehemu ya Tottenham Hale wenye jina la hapo juu. Ankal ametembelea hapo na kupata msosi wa nguvu wa wali wa nazi kwa samaki hapo chini
Before....
After.....
Wali wa nazi kwa samaki, me mate yamenitoka
ReplyDeletehahaha....mbona umekimbia mboga mboga?!
ReplyDeleteAnkali hujaacha hata sampuli! Ukigua tutapeleka nini maabara. Lakini huo ubwabwa, mhhh! Sio wa Mbeya au Ifakara...
ReplyDeleteMichuzi upo UK na kikwete, firwa kaka
ReplyDeleteMiye nafikiri najua kiswahili, lakini wakati mwingine maji yazidi kina, basi naomba tafsir au maelezo ya maoni ya ndugu yangu hapo juu anayesema Michuzi upo UK.....
ReplyDeletenamkumbuka FARIDA kutoka mikocheni mpaka uk biashara ya mama mtilie kweli maisha safari ndefu sana
ReplyDeletenipe adres kamili weekend hii nikale hapo na mimi
naona ankal una alegy na mboga mboga.umekomba ma-michuzi yote lakini mboga umeacha.moboga mboga ndiyo afya yenyewe ,najua ankal kila chakula ulacho lazima kuwe na ma-michuzi.
ReplyDeletehaa haa hongera uncle, umenikumbusha mbali Enzi za farida fashion show.
ReplyDelete