Jumapili
huwa ni siku muhimu sana kwa familia. Ni siku ambayo mama/dada anapata
nafasi ya kukaa ama kutembelea ndugu jamaa na marafiki. Kwa kufahamu
umuhimu wa kuwa na familia yenye furaha na upendo, PSI Tanzania
kupitia brand yao ya Familia wanakuletea Familia Kitchen Party Gala
tour,Dar es Salaam. Nafasi ya mwanamke wa Dar es Salaam kupata mafunzo
na kujinoa kuhusu mambo yanayomuhusu yeye,afya, saikolojia, kupanga
muda, na mengine meeengi.
Hii ni nafasi ya kina mama kupima Kansa ya mlango wa uzazi, kupata
mafunzo ya uzazi wa mpango na kufunzwa na Mama Victor, Aunt Sadaka na
Kaka Chris... huku kukiwa na burdani murua ya Malkia Khadija Kopa,
Kuserebuka na Mwasiti...na hata kuSugua gaga na Shaa!
Nunua Tiketi yako sasa kupitia vituo hivi;
1.Trudy's Intimate Apparel - Mwenge near Tamal Hotel
2.Shear
Illusions - Mlimani City, Millenium Towers
3.Jackz Cosmetics -
Kinondoni Muslem near Barclays
4.S.H Amon - Posta, Kariakoo
5.Cassandra Lingerie - Sinza Makaburini, Mikocheni kwa Nyerere,
Golden Jubilee
6.Lampard Cosmetics - Tandika
7.Amina
Designs - Kariakoo
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...