Katika siku za hivi karibuni, huko mkoani Mara wilaya ya Butiama kumejitokeza matukio ya mauaji yanayowalenga hasa akina mama wawapo katika shughuli zao mbalimbali.
Kufuatia matukio hayo, Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu ametuma timu maalum ya wataamu itakayoongozwa na Mkurugenzi wa Upelelezi wa makosa ya jinai nchini, DCI Issaya Mngulu kwenda mkoani humo kuongeza nguvu kwa kushirikiana na wataalam wa mkoa huo, ili kuhakikisha kwamba wote wanaojihusisha na vitendo hivyo wanakamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria haraka.
Jeshi la Polisi linawashukuru wananchi wanaoendelea kutoa ushirikiano utakaosaidia watuhumiwa hao kuendelea kukamatwa na linatoa wito kwa wananchi wa mkoa wa Mara na maeneo ya jirani kuwa watulivu wakati upelelezi ukiendelea.
Aidha, Jeshi la Polisi nchini linawaomba wananchi wenye taarifa za wahalifu hao kutoa taarifa hizo kupitia namba za simu zifuatayo; 0715 009930, 0754 785557 au katika kituo chochote cha Polisi.
.
Imetolewa na:
Advera Senso -SSP
Msemaji wa jeshi la Polisi.
Hivi ni sahihi kwa mkurugenzi wa makosa ya jinai kupelekwa kufanya kazi za kiupelelezi?
ReplyDeleteKwani mkurugenzi wa makosa ya jinai si ni askari kama askari wengine, ukurugenzi ni title tu, acha kiuliza masuali ya kiraia.
ReplyDeleteNdugu zetu wa Mkoa wa Mara ni wakorofi sana!
ReplyDeleteTazameni hadi eneo la Tarafa moja ya Rorya kufikia kupewa hadhi ya Mkoa wa Ki-Polisi sio kitu cha kawaida!
Mikoa ya Ki-Polisi imepewa Wilaya za Dar Es Salaam na siyo Tarafa kama ilivyotokea huko Mkoani Mara, hii ni kutokana na kuwa watu wa huko ni wakorofi na Wahalifu sugu.
Kwa miaka mingi sana watu wa Mara wamekuwa wakishiriki Uchumi wa Kilimo cha Bangi na Pombe ya Gongo na sasa kwa mauaji na unyama dhidi ya wa akina mama na wanawake watu wa Mara wamehamia kwenye Uwekezaji wa Imani za Kichawi!!!
Ndio maana tuna mitandao ya kijamii ili watu waweze kuelimishana hivyo usichangie ujuzi wako kwa hasira.
ReplyDeleteVilex2 Title ndio inayo mtofautisha mtu na mtu katika majukumu yake,hivyo sidhani km jibu lako linatoa jawabu kwa swali la enonymous #.1