Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba, Deus Kibamba akizungumza katika mkutano wa waandishi wa habari uliofanyika ofisi za Jukwaa la Katiba jijini Dar es Salaam katika kutoa tamko rasmi za tathimini ya Jukwaa la Katiba Tanzania kuhusu Katiba Mpya, Tulipotoka, Tulipo na Tuendako. Pembeni ni Msimamizi wa Mradi wa taasisi isiyo ya kiserikali ya (NGO Network for Dodoma) Bw. Edward Mbogo (kushoto) na Mjumbe wa Jukwaa la Katiba toka Pemba Bw. Omari Omari.

Waandishi wa Habari wakifuatilia.
---
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam.

Jukwaa la Katiba Tanzania (JUKATA) limejitolea kuratibu maridhiano miongoni mwa makundi ya kisiasa asasi za kiraia, asasi za wananchi na taasisi zote za muhimu zilizoguswa na migogoro inayoendelea katika Bunge maalum la katiba Tanzania.

Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za Jukwaa la Katiba jijini Dar es Salam, Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba Bw. Deus Kibamba juu ya tathimini walizozifanya katika bunge hilo wameamua kujitolea kufanya maridhiano hayo kwa kuwashirikisha viongozi maarufu Afrika Mashariki akiwemo mheshimiwa jaji mkuu mstaafu wa Tanzania, Barnabas Samatta ambaye atakuwa mkuu.

wa jopo hilo la usuluhisho na ndugu Patrice Lumumba kutoka nchini Kenya ambaye atakuwa msaidizi.
Aidha jukwaa hilo limeonyesha masikitiko yake kwa kile alichookiita ni uvunjifu wa kanuni mara baada ya wabunge zaidi ya mia mbili kutoka nje lakini wabunge waliobakia kuendelea kurekebisha kanuni za bunge hilo jambo ambalo wamesema kuwa haikustaili kwani wana uwezo wa kujitungia sheria.

Kibamba amesema kuwa kutokana na mwenendo wa bunge hilo hadi hapa lilipofikia wabunge hao hawana nia ya dhati ya kulipatia taifa katiba mpya huku akitolea mfano kuwa katiba mpya ilipangwa kuwekwa saini na Rais siku ya tarehe 26 mwezi huu yani leo lakini hadi sasa hata majadiliano ya sura mbili hayajamalizika, na kuwahakikishia watanzania kuwa hakuna katiba mpya itakayopatikana kwa mwaka huu.

Hata hivyo mwenyekiti huyo amewataka wajumbe wote na asasi zote zilizopo nje ya muendelezo wa bunge hilo maalumu la katiba kuwa tayari kwa maridhiano kwa mtu au taasisi yoyote atakayekuwa tayari kutatua migogoro yao ili kuwezesha upatikanaji wa katiba kwa taifa letu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Napendekeza kwanza tupige kura ya maoni (referendum) juu ya muundo wa serikali kabla ya kuendelea na mjadala hapo mwezi wa nane. Hawa wanasiasa sijui UKAWA sijui CCM siwaamini hata kidogo. Hawa wote wana ajenda zao za siri za kisiasa. Ubaguzi na uroho wa madaraka vimo ndani mwao. Kama kweli mnataka kujua wananchi wanataka serikali ngapi itisheni kwanza kura ya maoni. Twende tupige kura ya maoni, matokeo yake ndiyo yatakayo kata mzizi wa unafiki. Tume ya warioba imewahoji watu wachache sana. Tuacheni tupige kura. Mbona Zanzibar walipiga kura kuamua serikali ya kitaifa? Na sisi tupige kura kwanza kabla ya bunge la katiba halisonga mbele.

    ReplyDelete
  2. hili bunge ni upoteshaji wa pesa za nchi tu, hakuna linafanyika na hakuna litakalofanyika. wajumbe waliomo katika bunge hili wanafurahia marupurupu wanayokula kila siku na hawajali walala hoi

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...