Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohamed Mpinga ( aliyesimama) akifafanua kwa ufasaha vifungu vya sheria za usalama barabarani na miiko ya maadili ya udereva, wakati akifungua warsha ya mafunzo kwa maderva wa kampuni ya UDA jijini Dar es Salaam leo. Aliwafunda madereva hao kuwa wasafi, lugha nzuri na kutabasamu kwa abiria ambao ni wateja wao.Wengine pichani ni Mwenyekiti wa makampuni ya Simon Group,Robert Kisena (kulia) na David Mziray kutoka SUMATRA.
Mwenyekiti wa makampuni ya Simon Group,Robert Kisena (aliyesimama) akitoa neno la shukrani kwa Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohamed Mpinga aliyefungua warsha ya mafunzo kwa madereva wa UDA leo jijini Dar es Salaam.
Madereva wa UDA wakifurahia mafunzo ya sheria za Usalama Barabarani yaliyofunguliwa na Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mohamed Mpinga jijini Dar es Salaam leo.
Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohamed Mpinga (kushoto) akiteta jambo na Mwenyekiti wa makampuni ya Simon Group, Robert Kisena wakati wa warsha ya mafunzo ya madereva wa shirika la UDA jijini Dar es Salaam leo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...