Katibu Mkuu wa CCM;Ndugu Kinana na Wananchi wakishiriki ujenzi wa Ghala la kuhifadhi mazao na mashine ya kusaga nafaka katika kijiji cha cha Kidahwe,Kigoma Vijijini.Ghala hilo linalenga kusaidia katika kuhifadhi mazao ya wakulima na kijiji hicho baada ya kuvuna ili kusubiri soko na bei nzuri ya mazao kwa mfumo wa stakabadhi ghalani.Usimikaji wa mashine katika ghala hilo utawasaidia pia wakulima kuchakata mazao yao (hasa mahindi na muhugo) na kuuza unga badala ya mahindi.Gharama za mradi huo ni shiliingi milioni 104,800,000/=.
Katibu wa NEC-CCM wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akishiriki ujenzi wa Ghala la kuhifadhi mazao na mashine ya kusaga nafaka katika kijiji cha cha Kidahwe,Kigoma Vijijini.Ghala hilo linalenga kusaidia katika kuhifadhi mazao ya wakulima na kijiji hicho baada ya kuvuna ili kusubiri soko na bei nzuri ya mazao kwa mfumo wa stakabadhi ghalani.Usimikaji wa mashine katika ghala hilo utawasaidia pia wakulima kuchakata mazao yao (hasa mahindi na muhugo) na kuuza unga badala ya mahindi.Gharama za mradi huo ni shiliingi milioni 104,800,000/=.
Baadhi ya Wazee wa kijiji cha Nkungwe wakifuatilia yaliyokuwa yanazungumwa na Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana katika kijiji cha Nkungwe,kuhusiana na tatizo la ufumbuzi wa mradi wa maji.
Mjumbe
wa NEC,Balozi Ally Karume akifafanua jambo kwa Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu
Kinana mara baada ya kukagua mradi mkubwa wa maji katika kijiji cha
Nkungwe,Kigoma vijijini.Mradi huo umeshindwa kukamilika kutokana na
ukosefu wa fedha,lakini pia Kinana amewahidi wananchi kulitafutia
ufumbuzi wa haraka tatizo hilo na hatimaye mradi huo kukamilika na
kuwasaidia wananchi mbalimbali wa maeneo hayo.
Ndugu
Kinana akiwasalimia wananchi mbalimbali (hawapo Pichani),wakati
alipokuwa akiwasili katika kijiji cha Nkungwe kukagua mradi wa maji
ambao umeshindwa kukamilika kutokana na ukosefu wa fedha. Kinana
amewaahidi wananachi kulitafutia ufumbuzi suala hilo ili mradi huo
ukamilike na kuanza kutoa huduma kwa wananchi.
Ujenzi wa tanki hilo la maji kama lionekanavyo pichani.
Ndugu Kinana (wa tatu kulia),akishiriki kufukia mabomba ya mradi wa maji katika kijiji cha Nkungwe,Kigoma vijijini.Mradi huo ukikamilika unatarajiwa kusaidia vijiji zaidi ya 30.
Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akisoma orodha ya vijiji vitakavyopatiwa umeme
na maji katika wilaya ya Kigoma Vijijini. Kikiwemo Kijiji cha Mahembe
ambacho tayari kimepata umeme.
Katibu wa NEC-CCM wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye (katikati) akihutubia katika mkutano wa hadhara katika Kata ya Mahembe, Jimbo la Kigoma Kaskazini.
KWA PICHA ZAIDI BOFYA MICHUZIJR.BLOGSPOT.COM
KWA PICHA ZAIDI BOFYA MICHUZIJR.BLOGSPOT.COM
Hayo ndio maisha ya watanzania!!!!. Wabunge wa katiba badala ya kuokoa fedha wanataka kuongezewa muda ili waendelee kubishania mambo yasiyokuwa na tija wala msingi. Elekezeni fikra zenu kujenga uchumi wa nchi na si kubishania serikali. Ikiwa na serikali mbili au tatu zitaleta maendeleo? Angalieni uchumi wa nchi acheni mchezo wa vyama na kufikiria madaraka.
ReplyDelete