Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimsikiliza Mzee Masoud Mwinyi Chande kwenye mnara wa kumbukumbu ya nyumba ya kwanza ambayo Mwalimu Julius Nyerere alifikia Ujiji wakati akifanya harakati za kutafuta Uhuru, Inaelezwa kuwa Nyumba hiyo Mwalimu Nyerere alifika akiongozana na Suleiman Takadili na Bibi Titi Mohamed.Kulia ni Mbunge wa Kigoma Mjini,Mh Peter Serukamba,Katibu wa NEC,Siasa na Uenezi,Nape Nnauye,pamoja na Mwenyekiti wa CCM-Kigoma Ndugu Amani Kabouru. 
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akielekezwa sehemu ya Chumba na mlango ndani ya nyumba ya kwanza ambayo Mwalimu Julius Nyerere alifikia Ujiji wakati akifanya harakati za kutafuta Uhuru, Nyumba hiyo inasemekana Mwalimu Nyerere alifika akiongozana na Suleiman Takadili na Bibi Titi Mohamed.
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akipata maelezo mafupi ndani ya Nyumba ya Makumbusho ya Dr Livingstone iliyopo katika eneo la mji wa kihistoria,Ujiji mkoani Kigoma.
 Sehemu ya njia (route) kama ionekanavyo pichani ndani mji wa kihistoria Ujiji mkoani Kigoma,iliyotumika kusafirishia Watumwa kwenda sehemu mbalimbali,katika njia hiyo kuna miembe inayoelezwa ina umri zaidi ya miaka 150 tangu kupandwa kwake,na inaelezwa inapatikana sehemu ya Tabora na Bagamoyo. 
 Mmoja wa wakazi wa eneo la Kibiri,ambalo liko ufukweni kabisa mwa ziwa Tanganyika mkoani Kigoma,akibandika mabango yake yenye ujumbe wa kumpokea Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana,alipokwenda kutembelea eneo hilo na kusikiliza kero mbalimbali za wavuvi wadogo wadogo.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisoma bango lenye ujumbe wa kulalamikia kodi kubwa  wanazotozwa wavuvi wadogowadogo wa Kibirizi,Kigoma.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Kibirizi mkoani Kigoma ambao wanakilio cha kutozwa kodi kubwa, kuvamiwa na majambazi wakati wa shughuli zao za uvuvi.
Pichani Kati ni Mbunge wa Kigoma Mjini,Mh Peter Serukamba akieleza jambo kwa Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana (shoto) wakati wakielekea kutazama Nyumba ya Makumbusho ya Dr Livingstone iliyopo katika eneo la Ujiji mkoani Kigoma,kulia ni a Katibu wa NEC,Siasa na Uenezi,Nape Nnauye.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Kinana mwendo huohuo kwani mpaka sasa Wananchi wameanza kukukubali...

    ReplyDelete
  2. Gombea Urais baba

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...