Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana na baadhi ya viongozi wa chama Wilaya ya Kalambo,wakikatiza kwenye Ofisi ya CHADEMA,ambayo inadaiwa imefungwa yapata miaka mitatu sasa, kwa kushindwa kulipia pango.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akibeba tofali aliyoifyatua,ikiwa ni sehemu ya uzinduzi wa jengo la CCM,wilayani Kalambo.
Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiwahutubia wakazi wa kata ya Kasanga,iliopo
ndani ya wilaya mpya ya Kalambo,mkoani Rukwa mapema jana jioni.Kinana
bado yupo Mkoani Rukwa na ziara yake ya kuimarisha chama,kukagua miradi
mbalimbali,ikiwemo na kusikiliza kero za wananchi.
Baadhi
ya akina mama wakazi wa kata ya Kasanga wilayani kalambo wakishangilia
jambo,wakati Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana alipokuwa akizungumzia
mambo mbalimbali ikiwemo utatuzi wa masuala ya Afya,Elimu,Barabara na
maji.
Mjumbe
wa Halmashauri Kuu ya Taifa,Balozi Ally Karume akihutubia mbele ya
wananchi wa kijiji cha Kasanga kilichopo kando kando ya Ziwa Tanganyika,Wilayani Kalambo mkoani Rukwa mapema
jana,wakati wa mkutano wa hadhara.
Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akizawadiwa zawadi kutoka kwa akina mama wa
kata ya Kasanga,iliopo ndani ya wilaya mpya ya Kalambo,mkoani Rukwa.Kijiji cha Kasanga kipo kando kando ya Ziwa Tanganyika.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...