Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Iddi (Wapili kushoto) wakifurahia jambo katika mazungumzo na Spika wa Baraza la Wawakilishi, Pandu Kificho (wapili kulia) na Haidar Madeweyya .
Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba Mohamed Abood(kushoto) na Stephen Wassira wakibadlishana mawazo leo mjini Dodoma wakati wa kikao cha ishirini na mbili cha Bunge Maalum la Katiba.

Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Dodoma wakiwa Bungeni Mjini Dodoma Aprili 14, 2014 kwa ziara ya kujifunza.
Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba Sophia Simba (kushoto) na James Lembeli (katikati) na Job Ndugai (kulia) wakibadlishana mawazo leo mjini Dodoma wakati wa kikao cha ishirini na mbili cha Bunge Maalum la Katiba.
Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba Philemon Ndessamburo (kushoto) na James Mbatia (kulia) wakibadlishana mawazo leo mjini Dodoma wakati wa kikao cha ishirini na mbili cha Bunge Maalum la Katiba.
Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Samuel Sitta(wa pili kulia) akiongozana na wajumbe wengine wa Bunge hilo kuelekea katika mapumziko mafupi mara baada ya kikao kuharishwa leo mchana mjini Dodoma.
Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba James Mbatia (kushoto), Mohamed Raza( wa pili kushoto) , Profesa Ibrahim Lipumba (wa pili kulia) na Freeman Mbowe(kulia) wakibadlishana mawazo leo mjini Dodoma wakati wa kikao cha ishirini na mbili cha Bunge Maalum la Katiba. Picha na Bunge Maalum la Katiba -Dodoma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Hao wanafunzi wa Dodoma Sekondari hasa huyo mvulana mwenye suruali ya kijivu lazima atakuja kuwa mbunge maana ameanza mazoezi ya kusinzia Bungeni.

    ReplyDelete
  2. mwaka 2015 tunategemea
    1. tundu lissu- waziri wa sheria na mambo ya ndani
    2.profesa lipumba- waziri wa mipango na uchumi

    3. mtuhuru mbowe - wizara ya nje na ushirikiano kimataifa
    4. mbatia- waziri mkuu tanganyika

    5. isamil jussa - waziri mkuu zanzibar

    ReplyDelete
  3. mdau namba 1 umevunja mabvu zangu.
    mdau namba 2 hilo baraza la mawaziri halina hata rais?

    ReplyDelete
  4. Kwa duru za kisiasa zinavyokwenda mmoja umemkosea kumtabiria.Ismail Jussab atakuwa msahauliwa katika medani za kisiasa na nafasi yake kushikwa na Mansour Yussuf Himidi maana kukatika kwa patasi sio mwisho wa uhunzi. Usijeshangaa katika upepo wa mabadiliko,tusubiri tu bunge limalize kazi, maana huyu jamaa ni mtu mahiri,anajiamini na hababaiki na ana moyo kama wa marehemu baba yake.

    ReplyDelete
  5. nafikiri ameficha jina la raisi kwa ujanja kutuachia wadau wengine tufikiri

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...