Gavana wa Shirika la Lions Club nchini Bwana Wilson Ndesanjo akimvika Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete medali maalum ya Uongozi Bora na mahusiano mema wakati wa hafla fupi iliyofanyika ikulu jijini Dar es Salaam leo asubuhi.Bwana Ndesanjo alisema klabu hiyo imeamua kumtunuku Rais Kikwete medali hiyo kwa kutambua mafanikio makubwa yaliyopatikana nchini katika Nyanja mbalimbali kutokana na uongozi wake mahiri.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akipeana mkono na Gavana wa Shirika la Lions Club nchini Bwana Wilson Ndesanjo mara baada ya kuvalishwa medali maalum ya Uongozi Bora na mahusiano mema wakati wa hafla fupi iliyofanyika ikulu jijini Dar es Salaam leo
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa klabu ya Lions waliofika ikulu jijini Dar es Salaam leo kushiriki hafla ya kumtunuku Rais Kikwete medali maalumu ya Uongozi Bora na Mahusiano mema.(picha na Freddy Maro)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...