Meneja wa kanda ya Dar es salaam NMB, Bw. Salie Mlay akikabidhi kompyuta kwa Afisa elimu manispaa ya Temeke Bi. Honorina Mumba kwa ajili ya kituo cha walimu wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam. Msaada huu wa kompyuta mbili pamoja na mashine ya kuchapisha karatasi (Printer) vimetolewa na benki ya NMB kwa ajili ya mafunzo yanayotolewa kwa walimu katika wilaya hii.Hafla ya makabidhiano ilifanyika juzi jijini Dar es salaam. Akishuhudia makabidhiano hayo ni Mkuu wa kituo hicho cha walimu Temeke Bw.Daniel Matembele.
Meneja wa tawi la NMB Temeke Bw.Harold Lambileki akimkabidhi sehemu ya Kompyuta Mkuu wa kituo cha walimu Temeke Bw.Daniel Matembele. Msaada huu wa kompyuta mbili Pamoja na mashine ya kuchapisha karatasi (Printer) vimetolewa na benki ya NMB kwa ajili ya mafunzo yanayotolewa kwa walimu katika wilaya hii.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...