Lori lenye nambari za Usajili T 812 BQL lililokuwa na tela lenye nambari za Usajili T 738 ASH likiwa limepiga mweleka baada ya dereva wake aliejitambulisha kwa jina la Hamis Razack (24) kuzidiwa maarifa wakati akijaribu kuikwepa Bajaj iliyokuwa ikivuka barabara ya Mandera.Dereva wa Lori hilo amesema kuwa alijikuta akizidiwa maarifa na kujikuta akivuka ng'ambo ya pili ya barabara na kuja kujikita katika hapo.Ajali hii imetokea mchana wa leo maeneo ya Tabata Garage (gereji) wakati Lori hilo likitokea maeneo ya Buguruni na kuelekea Ubungo.hakuna aliepoteza maisha wala kujeruhiwa katika ajali hiyo.

Dereva wa Lori hilo aitwae Hamis Razack (24) akitoka kwenye Lori hilo huku akiwa haamini kilichomtokea mchana huu.
 Mashuhuda wakiliangalia lori hilo huku wakiwa hawaamini kile wanachokuona hasa kwa namna lori hilo lilivyoweza kuhama kutoka upande mmoja wa barabara na kwenda upande mwingine. 
 hivyo ndivyo hali ilivyokuwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Kungekuwa na soko la taka tungetajirika.

    ReplyDelete
  2. Hawa watu wa Bajajji na pikipiki wanatambia mbaya ya kuchomeka chomeka nashauri zipigwe marufuku kabisa kwenye highway zikae huko uchochoroni

    ReplyDelete
  3. Mbona kuna dampo hapo serikali za mitaa eneo hilo.

    ReplyDelete
  4. Ukiachilia hiyo bajaji, ukiangalia umri wa huyo kijana, hata kwa umbo tu na size ya lorry alilokuwa akiliendesha utagundua kabisa kuna suala la competence hapo, ujuzi wa huyo kijana unatia mashaka hata kwa umbali huo aliokwenda na kitendo cha kuvuka barabara upande wa pili. aidha unajiuliza kwa hali ya dar sijui alikuwa speed ngapi kiasi lorry kumshinda kiasi hicho

    ReplyDelete
  5. mjaribu kuangalia na umri wa madereva. Dereva wa lori ana miaka 24, huu ni umri mdogo sana kwa dereva kupewa jukumu la kuendesha gari kubwa kama hilo.

    ReplyDelete
  6. Madereva Bajaji ne kero tu nchi nzima sio wastaarabu kabisa

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...