Lori lenye nambari za Usajili T 812 BQL lililokuwa na tela lenye nambari za Usajili T 738 ASH likiwa limepiga mweleka baada ya dereva wake aliejitambulisha kwa jina la Hamis Razack (24) kuzidiwa maarifa wakati akijaribu kuikwepa Bajaj iliyokuwa ikivuka barabara ya Mandera.Dereva wa Lori hilo amesema kuwa alijikuta akizidiwa maarifa na kujikuta akivuka ng'ambo ya pili ya barabara na kuja kujikita katika hapo.Ajali hii imetokea mchana wa leo maeneo ya Tabata Garage (gereji) wakati Lori hilo likitokea maeneo ya Buguruni na kuelekea Ubungo.hakuna aliepoteza maisha wala kujeruhiwa katika ajali hiyo.

Dereva wa Lori hilo aitwae Hamis Razack (24) akitoka kwenye Lori hilo huku akiwa haamini kilichomtokea mchana huu.
Mashuhuda wakiliangalia lori hilo huku wakiwa hawaamini kile wanachokuona hasa kwa namna lori hilo lilivyoweza kuhama kutoka upande mmoja wa barabara na kwenda upande mwingine.
hivyo ndivyo hali ilivyokuwa.
Kungekuwa na soko la taka tungetajirika.
ReplyDeleteHawa watu wa Bajajji na pikipiki wanatambia mbaya ya kuchomeka chomeka nashauri zipigwe marufuku kabisa kwenye highway zikae huko uchochoroni
ReplyDeleteKweli mdau
DeleteMbona kuna dampo hapo serikali za mitaa eneo hilo.
ReplyDeleteUkiachilia hiyo bajaji, ukiangalia umri wa huyo kijana, hata kwa umbo tu na size ya lorry alilokuwa akiliendesha utagundua kabisa kuna suala la competence hapo, ujuzi wa huyo kijana unatia mashaka hata kwa umbali huo aliokwenda na kitendo cha kuvuka barabara upande wa pili. aidha unajiuliza kwa hali ya dar sijui alikuwa speed ngapi kiasi lorry kumshinda kiasi hicho
ReplyDeletemjaribu kuangalia na umri wa madereva. Dereva wa lori ana miaka 24, huu ni umri mdogo sana kwa dereva kupewa jukumu la kuendesha gari kubwa kama hilo.
ReplyDeleteMadereva Bajaji ne kero tu nchi nzima sio wastaarabu kabisa
ReplyDelete