Mkurugenzi wa Idara ya Haki za Binadamu, Bwana Francis Nzuki akifungua rasmi mafunzo ya stadi za uchunguzi yanayofanyika katika hoteli ya Naura Spring jijini Arusha. Mafunzo hayo ya wiki moja kuanzia Machi 31—4, 2014 yamelenga kuwaongezea maafisa wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) stadi za kiuchunguzi hasa wanapofanya uchunguzi unaohusiana na kazi za kila siku za Polisi. kushoto ni muwezeshaji kutoka Tume ya Haki za Binadamu ya Afrika Kusini Bibi. Lindiwe Khumalo na kulia ni Muwezeshaji Mkuu wa mafunzo hayo Bwana Sean Tait kutoka African Policing Civilian Oversight Forum (APCOF).Mafunzo hayo yamefadhiliwa na shirika la GIZ.
Sehemu ya washiriki wakiwa katika Mafunzo, wa kwanza kushoto ni Afisa Uchunguzi wa THBUB, Bwana Godian Binamungu na kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Msaada wa Sheria, Bwana Nabor Assey na anayeonekana kwa mbali ni Afisa Uchunguzi , Bi. Nancy Ngula.
Maafisa wa THBUB wakimsikiliza kwa makini Muwezeshaji Mkuu, Bwana Sean Tait (hayupo pichani).Kutoka kushoto ni Bibi Monica Marealle (katikati) ni Bwana Elias Sowani na (kulia) ni Bwana Pontian Kitorobombo.
Muwezeshaji Mkuu, Bwana Sean Tait akiongea na Maafisa wa THBUB wanaoshiriki mafunzo(hawapo pichani) na kuwataka kuwa wasikivu ili kwa pamoja waweze kupata faida kutokana na mafunzo hayo.Kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Haki za Binadamu, Bwana Francis Nzuki.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...