Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa(TFDA) Bw.Hiiti Sillo akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuhusu ukaguzi maalum wa maduka ya kuuzia vyakula “Supermarkets” na Mini-Supermarkets katika jiji la Dar es salaam kinyume cha sheria ya Chakula , Dawa na Vipodozi sura ya 219.
Mkurugenzi wa Usalama na Chakula wa TFDA Bw. Raymond Wigenge akitoa ufafanuzi kwa waandishi kuhusu hatua zinazochukuliwa na TFDA kuhakikisha usalama wa vyakula na Dawa nchini .TFDA imekuwa ikiongeza nguvu katika kukabiliana na bidhaa zisizokidhi viwango kwa kushirikiana na mamlaka nyingine za udhibiti kwa kukagua, kukamata na kuchukua hatua za kisheria ikiwemo kuwafikisha mahakamani wanaokiuka sheria.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa(TFDA) Bw.Hiiti Sillo (kulia) akitoa ufafanuzi wa baadhi ya bidhaa zilizokamatwa katika ukaguzi maalum kwenye maduka ya kuuzia vyakula “Supermarkets” na Mini-Supermarkets katika jiji la Dar es salaam zikiuzwa kinyume cha sheria ya Chakula , Dawa na Vipodozi sura ya 219. Wengine ni Mkurugenzi wa Usalama na Chakula wa TFDA Bw. Raymond Wigenge, na Meneja wa Ukaguzi wa Chakula wa TFDA kanda ya Mashariki Bw. Emmanuel Alphonce.
Afisa Uhusiano wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) akiwaonesha waandishi wa habari baadhi ya bidhaa zilizokamatwa na mamlaka hiyo zikiwemo chumvi, vinywaji, maziwa ya watoto ambazo hazijasajiliwa na mamlaka hiyo kufuatia ukaguzi maalum uliofanyika katika jiji la Dar es salaam.
Maziwa ya watoto aina ya SMA 1,2 na 3, Promil Gold, S-26 Gold, Nursoy, Progress Gold, Cow &Gate, Isomil 2 na Infacare Soya , Nutrikids na Aptimil 1 yaliyokamatwa ambayo hayajasajiliwa na TFDA .
Vinywaji baridi ambavyo havikusajiliwa na TFDA vilivyokamatwa kufuatia ukaguzi maalum katika jiji la Dar es salaam.Picha na Aron Msigwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. mimi naona huu ni mchezo wa kuigiza. hizo bidhaa zote zimetoka nchi za nje, TDFA ndio iliyopo mipakani, bandari na Airport. sasa inakuwaje wao wataaalam waachie viingie alafu watutake tusome, sisi tutajuaje..waletaji hawaandiki kuwa hiki kina madhara kwa binaadam, ni mpaka vipimwe..hatujasomea madawa na chakula tutajuaje?.. mimi nadhani, inatakiwa chombo kingine kichunguze hiyo TDFA yenyewe. imekuwa wachezaji na refariii ktk mchezo huo!
    maoni yangu MDAU.

    ReplyDelete
  2. Waonevu tu..Hamna lolote.

    ReplyDelete
  3. haimaanishi sio salama .... vina viwango vizuri tu.... ila tfda hamfanyi kazi ipasavyo ,nguvu ya soda nyie nani hawajui ?

    ReplyDelete
  4. Kwa jambo TFDA hawako sawa kabisa Hii process ya registration walitakiwa wafanye toka vitu havijaingia sokoni. Someni Kenya au India wanafanya nini. Na SIO bidhaa inaingia kwa walaji na imeshasambazwa nchi nzima, then nyinyi ndio mnatoa tamko. ina uwezekano hamfanyi kazi kwa karibu na taasisi nyingine kama TRA, Bandari nk. Mkubali kubadilika na kujifunza kutoka nchi nyingine. na sio kukimbia waandishi wa habari, wakati mapunguvu ya utendaji kazi ni yenu. Tanzania haina kiwanda cha vyakula vya watoto. kwa maana hiyo mlitakiwa mfanye ukaguzi na registration mapema sana. kwa hali hii inaonekana mna mapungufu makubwa sana katika utendaji wanu.

    ReplyDelete
  5. Du BBQ sauce nayo yawa kinywaji.
    mdau Ukerewe

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...