Frank Mvungi- Maelezo
WAZIRI wa wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Benard Membe anatarajiwa kuwa mgeni
rasmi kwenye mkutano wa Kimataifa wa Ualbino utakaofanyika mwezi Mei mwaka huu.
Hayo yamesemwa na Afisa Mahusiano na habari wa Chama cha Albino Tanzania (TAS), Josephat Torner
wakati wa mkutano na waandishi wa Habari leo jijini Dar es salaam.
Torner alisema mkutano huo wa siku moja utafanyika katika hoteli ya Serena Jijini Dar es salaam na
utawahusisha washiriki toka mataifa mbalimbali yakiwemo Nchi za Afrika Mashariki, Marekani, Nchi za
Ulaya na Nchi za Kusini mwa Afrika.
Alisema moja ya matarajio ya mkutano huo ni kupata sauti ya pana ya Kimataifa kuutaka Umoja wa
Mataifa kuitangaza tarehe 4 mwezi Mei kuwa Siku ya Kimataifa ya Ualbino.
Aliongeza kuwa lengo la maadhimisho ya siku hiyo ni kutafakari vikwazo vinavyosababisha tofauti ya
umri wa kuishi kati ya watu wenye ulemavu na watu wengine.
“Hii inatokana na ukweli kwamba kwa Tanzania wastani wa umri wa kuishi kwa watu wenye ualibino ni
miaka 30 wakati kwa watu wengine ni miaka 60”2, alisema Torner.
Alisema sababu zinazochangia watu wenye ulemavu wa ualbino kuishi nusu ya umri wa Watanzania
wengine ni kukabiliwa na saratani ya ngozi.
Alitoa wito kwa watu wote wenye ualbino,wazazi,walezi na wadau mbalimbali na umma kwa ujumla
kujitokeza kwa wingi katika maadhimisho haya.
Maadhimisho ya Siku ya Albino yalianzishwa hapa nchini mwaka 2006 na tangu mwaka huo yamekuwa
yakileta hamasa katika nchi mbalimbali Duniani.
Kilele cha maadhimisho hayo hapa nchini kinatarajiwa kuwa siku ya tarehe 4/5/2014 na kauli mbiu ikiwa
ni Haki ya Afya,Haki ya Uhai.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...