
Kwa mujibu wa taarifa kutoka eneo la tukio,inaeleza kwamba ajali hiyo
ilitokea majira ya saa 10 jioni jirani kabisa na kituo cha mafuta
kilichopo kando ya barabara ya Moshi-Arusha.
Taarifa kutoka eneo la tukio zimesema basi hilo lilipinduka wakati
likijaribu kupishana na magari yaliyokuwa yakitokea Arusha ambayo
yalianza safari bila ya kuwa na mpangilio hali iliyosababisha kutokea
kwa ajali hiyo.
Juhudi ya kumpata Kamanda wa polisi mkoa wa Kilimanjaro, ACP Robert Boaz zinaendelea kufanyika ili kuthibitisha idadi kamili ya waliojeruhiwa kwenye ajali hiyo. Tutaendelea kujilishana kadri taarifa itakavyokuwa ikitufikia.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...