Na Richard Bagolele,Chato
Mbunge wa jimbo la Chato na waziri wa Ujenzi Mhe. Dk. John Pombe Magufuli leo amekutana na baraza
la madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato kwenye ukumbi wa Halamshauri na kutoa zaidi ya
Shilingi Milioni 80 za mfuko wa Jimbo kwa kila kata kwa style mpya ambapo kila diwani ametaja mahitaji
yake na kupewa kiasi hicho kwa ajili ya kukamilisha miradi yenye nguvu za wa wananchi.
Tofauti na miaka mingine ambapo fedha hizo zimekuwa zikitolewa na kamati maalumu ya mfuko wa
jimbo ambaye Mhe. Mbunge ni Mwenyekiti wa kamati hiyo.
Katika hali ambayo haikutarajiwa na wengi Mhe. Magufuli amesikiliza hitaji la kila diwani kutoka kwenye
kata na kutoa sehemu ya fedha za mfuko wa jimbo ili kusaidia miradi ambayo tayari imeanzishwa kwa
nguvu za wananchi.
Madiwani hao walioanza kwa kila mmoja kutaja mahitaji yake hususani miradi ambayo imeanzishwa na
wananchi lakini imekwama katika hatua za umaliziaji Mhe. Magufuli alitoa kiasi cha fedha kisichopungua
Milioni moja kwa kila mradi ambapo kila diwani alikuwa na miradi zaidi ya mitatu.
“utaratibu huu ni mzuri, nimeamua kukutana na ninyi waheshimiwa madiwani ambao mnatoka kwa
wananchi ambako kuna miradi muniambie ili kila diwani anieleze matatizo yake, na nimeona utaratibu
huu ni mzuri kwani ningeweza kukaa na wajumbe wangu tukagawa hizi fedha tunavyotaka lakini leo
tunagawa bila upendeleo” alisisitiza waziri Magufuli.
Hata hivyo waziri Magufuli amewataka madiwani kwa kushirikiana na watendaji kuhakikisha fedha hizo
zilizotolewa na mfuko wa jimbo zinafanya kazi zilizokusudiwa tu na kuwaomba wazisimamie vyema.
Nao madiwani waliopata nafasi ya kuongea wakiwemo wa vyama vya upinzani walimshukuru waziri
Magufuli kwa utaratibu huo wa kugawa fedha za mfuko wa jimbo kwa kuwashirikisha madiwani wote
tena kwa uwazi mkubwa na wamemwahidi kumpa ushirikiano katika kuleta maendeleo kwa wananchi.
Naye mwenyekiti wa CCM wilaya ya Chato ndugu Ibrahim Bagura amemshukuru Mhe. Magufuli kwa
kitendo hicho cha kugawa fedha za mfuko wa jimbo kwa uwazi bila upendeleo wa vyama na kuwaomba
madiwani wazisimamie vyema fedha hizo.
Mhe.Dk. Magufuli akisoma taarifa ya fedha ambazo zimewahi kutolewa na mfuko wa jimbo
kwa wajumbe wa baraza la madiwani la Halamshauri ya Wilaya ya Chato.
Diwani wa kata ya Muganza Mhe. Michael Maduka akichangia katika kikao hicho.
Wajumbe wa baraza la madiwani wakimskiliza Mbunge wa jimbo la Chato Mhe. Dk. John
Magufuli.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...