Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (Mb.) (kushoto) akisalimiana na mmoja wa wajumbe anayewakilisha wafanyabiashara kabla ya kufungua kongamano la mafuta na gesi linaloendelea huko Ujerumani kama moja ya maadhimisho ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar
Mtaalamu kutoka Shirika la Maendeleo ya Petroli Nchini (TPDC) Bi Venosa Ngowi (kulia) akimweleza Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (mwenye suti nyeusi) shughuli zinazofanywa na shirika hilo kwenye maonesho yanayoendelea huko Berlin, Ujerumani. Pembeni ya Waziri ni Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani Mhe. Philip Marmo.
Mtaalamu kutoka Wakala wa Jiolojia Nchini (GST) Bi. Augustina Rutaihwa akitoa maelezo kwa Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (katikati) juu ya shughuli zinazofanywa na wakala huo. Kushoto mwa Waziri ni Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani Mhe. Philip Marmo.
Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani Mhe. Philip Marmo akifungua kongamano hilo.
Kikundi cha ngoma za sanaa kutoka Jeshi la Wananchi Tanzania kikitumbuiza kabla ya kuanza kwa kongamano hilo.
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo akifungua kongamano hilo ikiwa ni pamoja na kuwasilisha mada juu ya fursa za uwekezaji nchini Tanzania katika sekta za mafuta, gesi ikiwa ni pamoja na madini.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...